TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
WANACHAMA wa mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) wilayani Masasi wameulalamikia mfuko huo kwa kile walichodai kuwa ni kupewa huduma zisizolingana na gaharama ya pesa wanayochangia.
Aidha wameelezea kukerwa kwao na huduma hizo zinavyosuasua huku wakidai kuwa kumekuwa na foleni kubwa wanapokwenda kupata matibabu kwenye hospitali,vituo vya afya na zahanati.
Malalamiko hayo yametolewa na wanachama hao hii leo kwenye ukumbi wa miduleni wakati wa kikao cha tathimini ya mfuko huo pamoja na kupokea changamoto mbalimbali kutoka kwa wanachama.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye kikao hicho Mwajuma Abbasi ambaye ni mwalimu wa shule ya sekondari ya kutwa ya Mtapika,Prisca Mwiru na Majid Ruo walibainisha changamoto mbalimbali zinazoukabili mfuko huo na kuiomba NHIF kufanya maboresho ya huduma.
Kwa upande wake Ruo alisema kumekuwa na udhaifu mkubwa katika utunzaji wa kumbukumbu katika ofisi ya NHIF mkoa wa Mtwara mazingira yanayopelekea taarifa za baadhi ya wanachama kupotea au kutopatikana kwa wakati pale zinapohitajika.
Awali akijibu malalamiko ya wanachama hao meneja wa NHIF mkoa wa Mtwara Joyce Sumbwe alisema mfuko una nia nzuri ya kuhudumia wanachama wake ila wamekuwa wakikutana na changamoto mbalimbali kutoka kwa watoa huduma pamoja na wanachama wenyewe ambapo amewashauri wanachama kuulinda mfuko huo ili uwe na manufaa makubwa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD