Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

VIJANA WILAYANI MASASI WAFUNDWA KUHUSU UTAMBUZI WA VIUNGO VYA UZAZI KWA BINADAMU

TANGAZO
Na Clarence Chilumba,
Masasi.

VIJANA kutoka kwenye vikundi mbalimbali wilayani Masasi mkoani Mtwara wamepatiwa mafunzo ya utambuzi wa viungo vya uzazi kwa binadamu ili kuwa na uwelewa wa kutosha kuhusu usalama na athari za masuala ya uzazi kwa vijana.

Mafunzo hayo ya siku tatu yameratibiwa na shirika lisilo la kiserikali la Masasi Sports and Farming Association (MASAFA) lililopo wilayani hapa kwa ufadhili wa mashirika ya DSW, EVERPLAN na GIZ ambapo mafunzo yalifanyika katika ukumbi wa chuo cha utabibu mjini hapa.
Akitoa mada kuhusu afya ya uzazi mratibu wa kudhibiti ukimwi Halmashauri ya mji Masasi Andrew Mugezi alisema kuwa afya ya uzazi kwa vijana ni suala la msingi na kwamba elimu hiyo ya siku tatu itawasaidia vijana kutambua mfumo mzima wa viungo vyote vya uzazi alivyonavyo binadamu.
Alisema kundi la vijana ni kundi muhimu katika jamii hivyo linawajibu na kutambua viungo vya uzazi ambapo hatua hiyo itawafanya kufahamu namna ya kujilinda katika suala la afya ya uzazi hasa kuzitambua athari zinazojitokeza katika viungo vya uzazi kwa binadamu.
 Mugezi alieleza kuwa umuhimu wa kutambua viungo vya uzazi kwa vijana itawawezesha namna ya kuweza kujitunza katika mabadiliko ya kibinadamu ambayo yanahusisha afya ya uzazi ikiwemo kuzingatia usafi wa mwili na mavazi hasa kwa wavulana na wasichana.
Alisema zipo sababu nyingi ambazo kupitia viungo vya uzazi hasa kwa vijana wanatakiwa kuzingingatia ili kuufahamu mfumo wa uzazi na jinsi viungi vya uzazi vinavyotakiwa kulindwa na na kuchukua tahadhari katika kuvitumia hasa kwa vijana.
Kwa upande wake katibu wa shirika hilo la MASAFA, Amidu Chindamba alisema shirika hilo lina lengo la kuwafikia vijana wa kata mbalimbali za wilaya ya Masasi ili kuwapatia elimu mtambuka inayowalenga vijana ikiwemo ya ujasiliamali na elimu ya kujitambua katika maisha.
 Alisema kuwa mradi huo wa vijana unaoitwa kijana amka utawasaidia vijana katika kubadili tabia zao na kuweza kuwa katika mtazamo chanya wa maisha yao na kwamba umekusanya vijana ambao wako katika mfumo usioramsi.
Chindamba alisema wameanza na elimu ya uzazi kwa vijana hao kwa sababu elimu hiyo kwao ni muhimu kutokana na umri wao wanapaswa kutambua masuala ya uzazi ili watakapo ingia katika masuala ya mahusiano waweze kujinga na mambo mengi yanayohusu afya ya uzazi ikiwemo uzazi wa mpango.



 Mwisho                                          
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top