TANGAZO
Ofisa Miradi wa KIMAS Edward Biashara |
WALIMU
wa shule za msingi na sekondari halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara
wamehimizwa kutoa elimu ya afya za uzazi kwa wanafunzi ili kuwajengea uelewa wa
kutambua haki zao za msingi pindi
wanapokutana na changamoto mbalimbali katika masomo yao.
Wito
huo umetolewa leo na ofisa wa miradi wa shirika lisilo la kiserikali la KIMAS
Edward Biashara wakati wa semina ya siku
mbili kwa walimu wapatao 20 wakiwemo walimu 10 wa shule za msingi na walimu 10
wa shule za sekondari iliyofanyika
kwenye ukumbi wa KIMAS mjini hapa.
Shule
zilizoshiriki kwenye mafunzo hayo ya uanzishwaji wa klabu za haki za watoto mashuleni kwa
halmashauri ya mji wa Masasi ni pamoja na shule za msingi za
Mkuti,Masasi,Mtakuja,Matawale na McDonald ambapo kwa upande wa shule tano za
sekondari ni Anna Abdallah,Sululu,Mkuti Mix,Masasi Day pamoja na shule ya
sekondari ya kutwa ya Nangaya.
Biashara
alisema ni vyema walimu wakatumia fursa ya uanzishwaji wa klabu hizo za kwa
kuwaeleza wanafunzi umuhimu wa kutunza afya zao na namna ya kupambana na watu
ambao wamekuwa na tabia za kubaka pamoja na kulawiti watoto wenye umri mdogo.
Wakizungumza
na Blog ya Mtazamo Mpya nje ya ukumbi wa KIMAS mwalimu Joseph Chacha pamoja na
Kuwile Bruno waliishukuru KIMAS kwa kuandaa mafunzo hayo ambayo wamekiri watayatumia
vizuri katika ufundishaji wa namna ya kupambana na vitendo vyote vya unyanyasaji
na ukatili wanavyofanyiwa watoto ikiwemo
kazi ngumu,kubakwa na kulawitiwa.
Mafunzo
hayo ya siku mbili juu ya uanzishwaji wa klabu za haki za watoto mashuleni yameandaliwa na Kikundi Mwavuli Masasi KIMAS
na kufadhiliwa na shirika la terre De Homes Netherelands la nchini Uholanzi.
WALIMU wa shule za Msingi na Sekondari Halmashauri ya mji wa Masasi wakifuatilia kwa makini moja ya mada kutoka kwa Ofisa Miradi wa KIMAS Edward Biashara hii leo katika ukumbi wa KIMAS mjini Masasi.
MMOJA wa maofisa wa KIMAS (Mwenye Kompyuta) akiwa kwenye mafunzo ya uanzishwaji wa klabu za haki za watoto mashuleni.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD