TANGAZO
Mbunge wa Mtwara Mjini Asnain Murji. |
Na Haika Kimaro,Mtwara.
Mahakama kuu kanda ya Mtwara
imemtaka Mwenyekiti wa chama cha NCCR-MAGEUZI wilaya ya Mtwara mjini, Ulledi
Abdalla kumlipa mbunge wa Mtwara Mjini,Hasnei Murji (CCM) pesa kiasi cha
51.5 milioni kama gharama za kuendeshea kesi.
Hatua hiyo imekuja baada ya Mbunge
Murji kushinda katika
katika kesi ya madai ikiwa ni baada ya kushinda katika kesi ya pingamizi la
uongozi katika nafasi ya ubunge iliyokuwa imefunguliwa na Ulledi baada ya Murji
kutangazwa kama Mbunge katika jimbo hilo.
Awali katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2010 Ulledi alikuwa akiwania
jimbo hilo la Mtwara mjini kupitia chama cha CUF ambapo hakuridhishwa na
matokeo na kuamua kufungua kesi.
Akisoma shauri hilo mahakamani hapo ,Naibu msajili wa mahakama kuu
Mtwara, Hussen Mushi alisema ni wajibu
wake kusoma maamuzi kwa niaba ya msajili aliyekuwepo awali na ndipo aliposema
Ulledi anatakiwa kulipa gharama hizo na kama hajaridhika na maamuzi hayo
anaruhusiwa kuandaa reference judgement.
Awali mahakamani hapo Ulledi aliyewakilishwa na katibu wake
binafsi, Fatuma Sinani ambaye pia ni mjumbe wa halmashauri kuu ya taifa aliieleza mahakama kuwa
Ulledi kwa sasa yuko katika chuo cha kiislamu cha Morogoro na kwamba barua ya
kumtaka awepo mahakamani hapo aliipata juzi mchana wakati tayari alikuwa
ameshajiandaa kwa ajili ya kurudi chuo kufanya mitihani.
Hata hivyo baada ya kutoka mahakamani katibu huyo aliwaeleza
waandishi wa habari kuwa mahakama haikutenda haki na kwamba wataendelea kukata
rufaa.
“ Judgment nimeipokea tutakata rufaa haki haijatendeka kwani sisi
kesi tuliyoileta ni nyingine lakini imepindishwa,”alisema Sinani
Akizungumza Hussein Mtembwa wakili wa kijitegemea aliyekuwa
akimwakilisha wakili Peter Kibatala kwa niaba ya Murji mahakamani hapo
aliwaambia wanahabari kuwa
hiyo ilikuwa ni hukumu ndogo ya madai na mahakama iliona madai yao ni ya msingi
ndipo ilipotoa maamuzi ya kulipwa kwa kiasi hicho cha pesa.
“Ilikuwa ni hukumu ndogo ya madai na mahakama iliona madai yetu ni
ya msingi na hukumu ndio imetolewa anatakiwa kulipwa Sh 51.5 milioni , na kama
wataona kuna haja ya kuandaa reference ni haki yao cha msingi ni kufuata sheria
na taratibu,”alisema wakili Mtembwa.
Alipotafutwa mbunge huyo alisema kuwa mahakama ndio sehemu ya
mwisho ambapo haki hupatikana na kusema kuwa yote hayo yametokana na pingamizi
la ushindi wa ubunge katika jimbo analoongoza sasa na kudai kuwa mpinzani wake
huyo alikata rufaa hadi kufikia mahakama ya rufaa lakini bado mahakama imeona
ana haki ya kulipwa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD