TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
SERIKALI kupitia
wizara ya maliasili na utalii imesema iko kwenye hatua za mwisho za kukamilisha
mchakato wa kutoa vibali kwa wafanyabiashara watakaokuwa tayari kuvuna mamba
kwenye maeneo ambayo wananchi wake wamekuwa wakiuawa au kujeruhiwa na wanyama
hao waishio majini.
Kauli hiyo yenye
matumaini kwa wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya mito ikiwemo mto Ruvuma
wilayani Masasi imetolewa na waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu
wakati anazungumza na watumishi wa idara ya wanyamapori alipotembelea ofisi zao
wakati wa ziara yake wilayani Masasi mwishoni mwa wiki.
Nyalandu alisema
wamelazimika kuchukua hatua hizo kutokana na wanyama hao kujeruhi na kuua watu
na kwamba zoezi hilo la uvunaji wa mamba hao utafuata kanuni na taratibu zilizopo
huku akiweka wazi kuwa ofisa wa wanyamapori nchini atakayetumia vibaya kutolewa
kwa vibali hivyo atachukuliwa hatua kali za kisheria.
Alisema si busara
kuacha wananchi wakiendelea kupoteza maisha wakati serikali ikiona na kwamba
hatua hiyo inaonesha ni kwa jinsi gani serikali inawajali wananchi wake.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD