TANGAZO
Na
Sigfrid Binna,Newala
Mwenyekiti
wa Chama Chama Mapinduzi Mkoa wa
Mtwara Mohamed Sinani amewataka wananchi wilayani Newala kuondoa
hofu juu ya upatikanaji wa pikipiki zao walizochangia fedha kutokana na kuwepo kwa taarifa za kutapeliwa
miongoni mwa wachangiaji hao.
Akizungumza
na Blog ya Mtazamo Mpya kwa njia ya simu alisema hakuna wizi wala utapeli katika suala hilo na
kwamba kinachochelewesha kupatikana kwa pikipiki hizo ni kutokana na mzabuni aliyepewa kazi ya kusafirisha kutoka nchini China kushindwa
kusafirisha kwa wakati kwa kile alichokieleza ni sababu zilizo nje ya uwezo
wake.
Kwa
mujibu wa mwenyekiti huyo wa CCM mkoa wa Mtwara alikiri kupata taarifa za kuwepo kwa wasiwasi
kutoka kwa wachangiaji hao wilayani humo mazingira yaliyopelekea baadhi
ya wananchi waliochangia kukutana na
Mchumi wa Chama cha Mapinduzi wilaya ya
Newala Jamali Nandonde ili kujua
mustakabali wa suala hilo.
Alisema
mchumi huyo wa Chama wilayani humo amemuonesha risiti pamoja na viambato vyote
muhimu vya manunuzi ya pikipiki hizo.
Aidha
amefafanua kuwa suala hilo liko wazi na
kwamba linafahamika na kufuatiliwa na
Chama hicho katika ngazi ya Taifa ambapo Katibu wa wabunge wa CCM Kisanga
analifuatilia kwa karibu ili liweza kupata ufumbuzi.
Chama
Cha Mapinduzi wilayani Newala kiliadhimia kukopesha pikipiki kwa riba nafuu,
kwa wananchi wilayani humo mwishoni mwa mwaka jana kwa kuchangia kiasi kidogo cha pesa na
kurudisha kidogo kidogo Pikipiki ambazo
zilitarajiwa kukabidhiwa februari mwaka huu ambazo mpaka sasa hazijafika kwa
walengwa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD