TANGAZO
Mkuu wa mkoa wa Lindi Mwamtumu Mahiza |
Na
Mwandishi wetu,Liwale.
Mkuu wa Mkoa
wa Lindi Mwamtumu Mahiza amewaagiza
wakurugenzi watendaji wa halmashauri za wilaya Mkoani humo ambao wameshindwa kutoa zawadi kwa wafanyakazi
bora kutoa maelezo ya kina ni kwanini
wameshindwa kutoa zawadi hizo huku wakijua kuwa ni wajibu wao.
Agizo hilo
limetolewa jana wakati wa kilele cha maadhimisho ya siku ya wafanyakazi Duniani
ambazo kimkoa zimefanyika wilayani Liwale ambapo alisema kitendo hicho
kilichofanywa na wakurugenzi hao ni aibu na kushindwa kutimiza majukumu yao.
Wakurugenzi
walioshindwa kutoa zawadi kwa wafanyakazi wao bora ni pamoja na halmashauri za wilaya za Ruangwa, Manispaa ya
Lindi, Lindi Vijijini,Nachingwea pamoja na Liwale huku wafanyakazi hao wakiambulia
kupewa vyeti na hundi hewa ambazo hazikusainiwa.
Mkuu huyo wa
mkoa wa Lindi ambae alikuwa mgeni rasmi katika sherehe hizo aligundua uonevu wa
wakurugenzi hao baada ya kuwataka
watumishi wote ambao ni wafanyakazi bora kufungua bahasha zao ili kuona
kilichopo ndani ya bahasha hizo ambapo
ilibainika kuwa hundi hizo hazijasainiwa.
Kati ya hundi
hizo ni hundi za halmashauri za wilaya
ya Nachingwea na Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa kutoka idara ya Afya ndizo
pekee ambazo zilikuwa zimesainiwa kwa ajli ya malipo.
Kutokana na
hali hiyo Mkuu huyo wa Mkoa wa Lindi
alitoa agizo kwa wakurugenzi wote walioshindwa kutoa zawadi kwa
wafanyakazi bora kwenda ofisini kwake wakiambatana na wakuu wa idara husika na
wafanyakazi waliokosa zawadi ili kwenda kutoa maelezo ni kwa nini wameshindwa
kutoa zawadi.
Akiongea kwa
Masikitiko makubwa na Blog ya Mtazamo Mpya mwenyekiti wa Chama cha Walimu wilaya
ya Ruangwa Rafael Soko alisema tabia
hiyo kwa wakurugenzi hao imekuwa ya kawaida kwao ambapo kila mwaka wafanyakazi
bora wamekuwa wakipewa hundi hewa ambazo huchukua zaidi ya miezi mitatu hadi
minne kukamilika kwa malipo.
Alisema
inashangaza kuona hali hii inajitokeza kila mwaka huku halmashauri hizo zikidai
kuwa kila mwaka huwa zinatenga fedha kupitia bajeti zake kwa ajili ya kutoa
zawadi hizo kwa wafanyakazi bora ndani ya halmashauri hizo.
Kwa upande wake kiongozi wa Talgwu wilaya ya
Ruangwa Bakari Ajuae alisema mwaka ujao
hatoruhusu Wanachama wake kwenda kwenye sherehe ya meimosi kabla ya malipo yao
kukamilika kwani kinachofanywa na wakurugenzi hao si kitendo cha kiungwana.
Alisema kwa mujibu
wa makubaliano na wakurugenzi hao mkoani humo kila mfanyajazi bora kwa mwaka 2015 alitakiwa
kupewa zawadi ya fedha isiyopungua shilingi laki nne za kitanzania.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD