TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
MICHUANO ya mbuzi
Cup imeendelea tena leo kwenye uwanja wa
shule ya Msingi Likangara wilayani Ruangwa katika hatua ya Robo fainali iliyozikutanisha
timu ngumu Bodaboda fc dhidi ya mahasimu wao wa muda mrefu Verona fc.
Mchezo huo
mkali na wa kusisimua ulianza kwa
kuchelewa pale timu hizo kutofika uwanjani kwa wakati uliopangwa kutokana na sababu
mbalimbali ambazo maofisa wa habari wa timu hizo walikana kuzitaja mbele ya
waandishi wa habari.
Katika mchezo huo uliojaa kila aina za
manjonjo kutokana na umaarufu wake walikuwa ni bodaboda fc walioanza kupata bao
la kwanza lililowekwa kambani na mshambulizi wa timu hiyo Shaabani Stambuli dakika
ya 36 baada ya kuiadaa ngome ya ulinzi ya timu ya Verona na kuachia shuti Kali lililomshinda
Mlinda mlango Makaki Ruvanga na kujaa kimiani.
Baada ya
kupatikana kwa goli hilo Verona Fc walijitahidi kupeleka mashambulizi ya mara
kwa mara langoni kwa Bodaboda Fc lakini uimara wa golikipa wa Bodaboda Fc
uliwafanya Verona wasipate bao hivyo hadi dakika 45 za mwanzo Bodaboda Fc
walikuwa wanaongiza kwa goli moja.
Kipindi cha pili kilianza kwa kasi huku timu
zote zikishambuliana kwa zamu lakini uimara wa safu ya ulinzi ya Bodaboda Fc iliyoongozwa na Hayaishi Boko bado
kilikuwa kikwazo kwa Verona Fc kuweza kusawazisha bao.
Huku watazamaji
wakiamini kuwa mchezo ungemalizika kwa
ushindi wa bao moja bila majibu alikuwa ni shaaban Stambuli tena aliyewainua
vitini mashabiki wa bodaboda fc kwa
kupachika bao safi na la ushindi kwa
mkwaju mkali katika dakika ya 87 ya
mchezo huo hivyo hadi filimbi ya mwisho
ya mwamuzi Bodaboda iliibuka kidedea kwa ushindi wa bao mbili bila majibu.
Kesho michuno
hiyo itaendelea katika mchezo mwingine wa robo fainali ya pili kwa kuzikutanisha
timu za Beach Boys na Iraq fc
Michuano hiyo ya
kugombea Mbuzi maarufu Mbuzi Cup ilianza kutimua vumbi mwaka huu ambapo jumla
ya timu nane zinashiriki michuano hiyo inayofanyika katika uwanja wa shule ya
msingi Likangara wilayani Ruangwa.
Timu
zinazoshiriki katika michuano hiyo ni pamoja na Likangara fc,.Mtota fc,.wavyuma
fc,.Iraq fc. Bodaboda fc,wachezapool fc pamoja na Verona fc.
Kwa mujibu wa muandaaji wa michuano hiyo Hasan Madebe alisema bingwa atajinyakulia zawadi ya Mbuzi, mshindi wa pili atajinyakulia kitita cha shilingi 40,000/= ambapo timu itakayoshika nafasi ya tatu itapata fedha shilingi 20000/=.
Mechi ya Ufunguzi katika michuano hiyo ilikuwa ni kati ya Likangara fc waliotoana
jasho na wavyuma fc ambapo mchezo
ulimalizika kwa sare ya bao 2-2 huku
wafungaji kwa upande wa Likangara wakiwa ni Denis Onesmo aliyefunga kwa mkwaju wa penati dakika ya 22 na bao la
pili la pili la Likangara Fc likiwekwa kimiani na Karimu Bakari dakika ya 29 ya
mchezo huo na kwa upande wa timu ya .wavyuma fc magoli yao yalisukumizwa kambani
na Saidi Mohamedi Mkalomba kwa njia ya penalt.
.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD