TANGAZO
Na Bashiru Kauchumbe,Ruangwa.
Michuano ya kombe la
Mbuzi wilayani Ruangwa imeendelea tena
leo kwenye uwanja wa shule ya msingi
Likangara ikiwa ni hatua ya nusu fainali
kwa kuzikutanisha timu ngumu za Likangara fc na Bodaboda zote zikiwa ni za wilayani humo.
Mchezo ulianza kwa
kasi huku kila timu ikihitaji ushindi hata hivyo walikuwa Likangara fc
waliokuwa wa kwanza kujipatia bao kunako dakika ya 45 kupitia kwa mshambuliaji
wake Godwin Geofrey aliyewalaba chenga walinzi wa timu hiyo na kupachika bao la
kwanza.
Kipindi cha pili
kilianza kwa timu ya Bodaboda kucheza kwa kasi huku wakihaha kupata bao la
kusawazisha lakini kama wasemavyo wahenga kuwa mbuzi wa masikini hazai
,Bodaboda walijikuta wakitandikwa bao la pili kwa mpira wa adhabu ndogo
uliochongwa na Joseph Mpili na kutinga nyavuni baada ya kumshinda mlinda mlango
Cosmas Chaitupu.
Adhabu hiyo
ilitolewa baada ya mchezaji shabani Manzi kufanyiwa madhambi nje kidogo
na eneo la hatari la timu ya Likangara Fc.
Mnamo dakika ya 80
ya mchezo Bodaboda fc walifanya shambulizi kali kutoka winga ya kulia ambapo mchezaji Hamisi Chikawe
aliyekuwa na mpira alifanyiwa madhambi
na Beki wa Likangara eneo la hatari na Mwamuzi wa mchezo huo Musa Chamtima alitoa
adhabu ya penati.
Penati hiyo nusura
ivunje pambano kwani ililalamikiwa na
wachezaji wa Likangara fc,hata hivyo mwamuzi hakuweza kubadili maamuzi yake na kuamuru
penati hiyo ipigwe kuelekea lango la
Likangara penati ambayo ilipigwa kiufundi
na mchezaji Hasani Mineng'ene na kuikwamisha kimiani na kuandika bao la kufutia
machozi
Zikiwa zimebakia
dakika tano kumalizika kwa mpambano huo Mwamuzi alimzawadia kadi nyekundu
Mlinzi wa Bodaboda fc Hayaishi Boko kwa
kumchezea vibaya Mchezaji Godwin Geofrey wa Likangara fc.
Kwa upande wao
baadhi ya mashabiki waliojitokeza kushuhudia mchezo huo walimlalamikia mwamuzi hasa baada ya kushindwa kutoa kadi Nyekundu
kwa Mchezaji Shabani Stambuli ambae alimpiga kwa makusudi ngumi ya usoni Juma stone wa Likangara fc na
badala yake alitoa kadi ya njano ,
Hadi filimbi ya
mwisho Likangara fc bao 2 Bodaboda bao 1 kesho kutakuwa na mchezo mwingine wa
nusu fainali ambao utawakutanisha wavyuma fc ambao watamenyana na Beach Boys
zote za mjini Ruangwa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD