Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA RASMI HII LEO MKOANI MTWARA KIJIJI CHA LUMESULE,NANYUMBU...

TANGAZO
 Na Clarence Chilumba,Nanyumbu.
MWENGE wa Uhuru umepokelewa rasmi hii leo majira ya saa 4:00 katika kijiji cha Lumesule kilichoko wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara.
Mwenge huo ulikuwa unatokea katika wilaya ya Tunduru mkoani Ruvuma na kuwasili viwanja vya shule ya msingi Lumesule na kupokelewa kwa furaha na nderemo kutoka kwa wakazi wa wilaya ya Nanyumbu na vitongoji vyake.
Makabidhiano ya mwenge huo wa uhuru yalifanyika baina ya kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Norman Sigala na Mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
Mwenge huo utakimbizwa katika wilaya zote sita mkoani Mtwara.

 KIONGOZI wa mbio za Mwenge kitaifa 2015 Juma Hatibu Chumu kutoka kusini Pemba wakati anaongea na wananchi wa kijiji cha Lumesule wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kati ya mkoa wa Ruvuma na Mtwara hii leo.
 Juma Hatibu Chumu,kiongozi wa mbio za mwenge mwaka huu akisalimiana na mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego hii leo wakati wa makabidhiano ya mwenge huo kwenye viwanja vya shule ya msingi Lumesule wilayani Nanyumbu.
 WAKIMBIZA mwenge kitaifa pamoja na Makamanda wa jeshi la polisi kutoka Wilaya ya Tunduru Mkoani Ruvuma wakiwasili kwenye viwanja vya shule ya msingi Lumesule.
 WAKUU wa wilaya za mkoa wa Mtwara wakiwa kwenye viwanja vya shule ya msingi Lumesule wakisubiri kuwasili kwa mwenge viwanjani hapo hii leo asubuhi.Kutoka kushoto ni mkuu wa wilaya ya Nanyumbu Sauda Mtondoo,mkuu wa wilaya ya Mtwara Fatma Ally,mkuu wa wilaya ya Newala Christopher Magala,Mkuu wa wilaya ya Tandahimba Emanuel Ruhaula na mkuu wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta.
 MKUU wa wilaya ya Tunduru Bakari Nalicho akimkabidhi mwenge wa uhuru kaimu mkuu wa mkoa wa Ruvuma Norman Sigala hii leo katika kijiji cha lumesule kabla ya kaimu mkuu huyo wa mkoa wa Ruvuma kumkabidhi mkuu wa mkoa wa Mtwara Halima Dendego.
 KATIBU Tawala wa mkoa wa Mtwara Alfred Luanda akipokea mwenge wa uhuru kutoka kwa mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa.
 KIONGOZI wa Mbio za Mwenge kitaifa Juma Hatibu Chumu akivishwa skafu kutoka kwa vijana wa chipukizi wilayani Nanyumbu mara baada ya kukabidhiwa kwa mwenge kwa mkoa wa Mtwara.
 KIONGOZI wa mbio za Mwenge akisalimiana na mkuu wa wilaya ya Nanyumbu mkoani Mtwara Sauda Mtondoo.
 BAADHI ya wananchi wa kijiji cha Lumesule waliojitokeza kushuhudia tukio hilo la kihistoria la kukabidhiwa kwa mwenge wilayani Nanyumbu.
 MWENYEKITI wa Halmashauri ya mji wa Masasi Andrew Mtumusha walikuwa ni miongoni mwa watu waliojitokeza kuupokea mwenge wa uhuru.
 MAKAMANDA wa Mbio za Mwenge wakiruka kuonesha ishara ya heshima kwa mwenge wa Uhuru mara baada ya kuwasili kwenye viwanja vya shule ya msingi Lumesule hii leo.
 MKUU wa wilaya ya Nanyumbu Sauda Mtondoo akisoma taarifa fupi ya wilaya hiyo kwa kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru  kitaifa Juma Hatibu Chumu.
MKUU wa wilaya ya Nanyumbu Sauda Mtondoo  akiwa na mwenge wa Uhuru. 
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top