TANGAZO
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego |
Na Fatuma Maumba,Mtwara
WAKURUGENZI wa
Halmashuri zote Nchini zinazolima zao la korosho wametakiwa kutumia vizuri
fedha zinazotarajiwa kutolewa na Mfuko wa kuendeleza zao la korosho kwa malengo
yaliyokusudiwa.
Rai hiyo ilitolewa
jana na Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego katika uzinduzi wa usambazaji wa
Pembejeo za Ruzuku zao la Korosho kwa ajali ya msimu wa kilimo 2015/2016
iliyofanyika katika viwanja vya mashujaa mjini hapa.
Dendego alisema
kuwa mfuko huo wa wakfu
unatarajia kutoa fedha kiasi cha shilingi Milioni 947,092,681 kwa mikoa na
halmashauri hivyo zitumike katika
shughuli za ufuatiliaji wa mwenendo wa usambazaji wa pembejeo.
Alisema kuwa fedha
hizo pamoja na matumizi mengine ya kuendeleza zao hilo zitumike katika
kuwafuatilia mawakala ambao si waaminifu wafuatiliwe ili kuwabaini na
kuwachukulia hatua za kisheria zinazostahiki.
“kwa vile hawa mawakala wanateuliwa na halmashauri husika, kwa
vyovyote vile mawakala hawa wanafahamika utendaji wao unajulikana hivyo
wanahitaji ufuatiliaji wa ukaribu zaidi katika usambazaji wa pembejeo hizi.”
Alisisitiza Dendego
Kwa upande wake katibu
mtendaji wa Mfuko huo Selemani Lenga alieleza kuwa kwa msimu huu 2015/2016
jumla ya tani 8000 za salfa ya unga zimenunuliwa ikiwa ni ongezeko la Asilimia
37.5 kutoka kiasi cha wastani wa tani 5000 kwa msimu uliopita.
Aidha Lenga alisema kuwa mpango huu wa pembejeo za Ruzuku
umewekewa muongozo maalumu na kila mdau amepewa majukumu yake ikiwemo
Sekretarieti ya Mkoa ,halmashauri za wilaya pamoja na serikali za vijiji
kuhakikisha pembejeo zinawafikia walengwa kwa wakati.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD