Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

MILIONI 3 ZAKUSANYWA UJENZI WA OFISI YA MTANDAO WA POLISI WA KIKE TANZANIA WILAYA YA MASASI

TANGAZO
Mwenyekiti wa TPF-NET mkoa wa Mtwara Mariamu Emanuel. 
Na Clarence Chilumba,Masasi.
JUMLA ya shilingi Milioni 3 zimekusanywa katika harambee ya ujenzi wa ofisi ya mtandao wa polisi wa kike Tanzania (TPF-NET) wilaya ya Masasi kwenye tafrija fupi iliyofanyika jana usiku kwenye ukumbi wa Kibo mjini hapa na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali walioalikwa.
 Katika harambee hiyo  iliyoongozwa na mwenyekiti wa TPF-NET mkoa wa Mtwara Mariamu Masalu  jumla ya shilingi milioni 3 zikikusanywa huku taslimu ikiwa ni shilingi 900,000 na ahadi ni shilingi milioni 2 pamoja na ahadi ya bati 18 na mifuko ya saruji minne.
Harambee hiyo ni kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya mtandao wa TPF-NET wilaya ya Masasi ambao hadi sasa hauna ofisi ya kufanyia kazi zake mazingira yanayopelekea kushindwa kufanya kazi kwa uhuru pindi kunapotokea waathirika wa matukio ya unyanyasaji wakiwemo wanawake na watoto ambao mahojiano yao yanatakiwa kuwa ya siri.
Akizungumza wakati wa harambee hiyo Masalu alisema fedha iliyopatikana ni lazima itumike kwa malengo yaliyokusudiwa ambapo jukumu la ujenzi wa ofisi hiyo liko chini ya mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Masasi Azaria Makubi kwa kushirikiana na uongozi wa jeshi hilo mkoa wa Mtwara.
Kwa upande wake mkuu wa jeshi la polisi wilaya ya Masasi Azaria Makubi aliwashukuru wadau wote waliojitokeza kuchangia michango hiyo na kwamba ofisi itajengwa ili kurudisha imani kwa waliotoa michango yao.
ASKARI wa kike wilaya ya Masasi wakicheza muziki wakati wa hafla fupi ya uzinduzi wa Mtandao wa polisi wa kike Tanzania wilaya ya Masasi kwenye ukumbi wa Kibo Pub mjini Masasi hapo jana.
 SEKRETARIET ya TPF-NET mkoa wa Mtwara nao haikuwa nyuma katika kusakata rhumba+vidole juu mambo ya pwani.
 HAPO SASA!!!! Ni WP-Pendo Pakacha mwenye simu mkononi akiwa na wenzake wakicheza "KWAITO" kwenye hafla fupi ya uzinduzi wa TPF-NET wilaya ya Masasi kibo pub.

 MWENYEKITI wa TPF-NET mkoa wa Mtwara Mariamu Emanuel akiongea wakati wa harambee ya ujenzi wa ofisi ya Mtandao wa polisi wa kike Tanzania wilaya ya Masasi jana usiku kwenye ukumbi wa kibo pub mjini Masasi. Kushoto kwake waliokaa ni Mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Masasi Beatrice Dominick na Mkurugenzi wa halmashauri ya mji wa Masasi Fortunatus Kagoro.
 NI FULL SHANGWE BAADA YA MAWP MASASI KUWEKA SILAHA CHINI NA KUSEREBUKAAAAAAAAAAAAAAA!!!!!!!!!!!!!
 WAKUZIBA INTERNATIONAL NAE ALIKUWEPO WAKATI WA SHEREHE HIZO ZA UZINDUZI WA TPF-NET WILAYA YA MASASI.

NANI KAMA MAMA!!!!
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top