TANGAZO
WAZIRI wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu ameapa kula sahani moja na majangili nchini licha ya kukiri kuwa mtandao wa majangili ni mkubwa na kwamba wote wanaotiwa mbaroni na vikosi vya askari wa wanyamapori hutumwa na watu waliopo kwenye ofisi za serikali na hata wengine kutoka nje ya nchi.
Pia
amewaagiza maofisa wanyamapori na misitu nchini kufanya kazi zao kwa kufuata
kanuni na taratibu za nchi na kwamba waache kufanya kazi kwa mazoea ambapo
amewaagiza kutoka sasa wamkamate mwananchi yeyote atakayevamia hifadhi za
wanyamapori zilizotengwa.
Nyalandu
ametoa maagizo hayo leo wakati wa ziara yake wilayani Masasi mkoani Mtwara alipokuwa
akizungumza na wafanyakazi wa idara ya wanyamapori,viongozi wa chama cha
Mapinduzi,wakuu wa idara pamoja na kamati ya ulinzi na usalama wilayani hapa.
Alisema
ujangili ni tishio kubwa kwa wanyamapori nchini na kwamba serikali kwa
kushirikiana na wizara ya mambo ya ndani,wizara ya sheria na wizara ya
maliasili na utalii imeandaa mpango mkakati wa kukabiliana na tatizo hilo la
ujangili linaloathiri sekta ya utalii nchini.
Kwa
mujibu wa waziri huyo alisema wizara ya maliasili na utalii kwa kushirikiana na
shirika la polisi la kimataifa “Interpool” pamoja na idara ya wanyamapori
watahakikisha wanawasaka majangili wote duniani lengo likiwa ni kukomesha
vitendo hivyo.
Alisema
Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizobahatika kuwa na idadi kubwa ya wanyamapori
lakini kutokana na vitendo vya ujangili vinavyofanywa na watu wasioitakia mema
nchi hii idadi ya wanyama imeendelea kushuka na kwamba hali hii ikiachwa
iendelee ni dhahiri kuwa misitu na mapori yatabaki wazi bila wanyama.
WAZIRI wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu akishika moja ya baadhi ya vipande 89 vya meno ya Tembo vyenye uzito wa kilogramu 222.1 vilivyokamatwa Oktoba 29,2013 majira ya saa 1;00 Asubuhi katika barabara ya Tunduru-Masasi eneo la Maendeleo kata ya Mkomaindo Tarafa ya Lisekese vikiwa ndani ya gari lenye namba za usajili T 867 BWX Toyota Carina.
Baadhi ya Vipande vya meno vilivyokamatwa na Kikosi cha askari wa wanyamapori wilayani Masasi ambavyo kwa sasa vimehifadhiwa kwenye ofisi za maliasili wilayani Masasi.
WAZIRI Nyalandu akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Masasi Kazumari Malilo mara baada ya kuwasili uwanja wa ndege huko katika kijiji cha Mbonde wilayani Masasi.
Mhifadhi mkuu wa wanyamapori wilaya ya Masasi akimuonesha waziri wa maliasili na utalii Lazaro Nyalandu ngozi ya Mamba,chui pamoja na simba zilizopatikana baada ya majangili kuua wanyama hao kwenye hifadhi za wanyamapori wilayani Masasi.
VITU ambavyo vimekamatwa na askari wa wanyamapori wilayani Masasi ikiwemo Mitego ya Panya,Baiskeli,Nyavu,Waya za kutegea wanyama pamoja na misumeno.
Mitego ya Panya iliyokamatwa na askari wa wanyamapori
WAZIRI wa Maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa idara ya wanyamapori mara baada ya kuongea nao alipotembelea kwenye ofisi hizo wilayani Masasi hii leo. Wa pili kulia kwake ni Mbunge wa Jimbo la Masasi Mariamu Kasembe.
Waziri Nyalandu akisalimiana na maofisa wa kamati ya Ulinzi na usalama ya wilaya ya Masasi wakati alipowasili uwanja wa ndege mjini Masasi.
Nyalandu akiangalia Baiskeli zilizokamatwa wakati wa operesheni Tokomeza zilizokuwa zikitumika kubebea mbao.mkaa na meno ya tembo.
WAZIRI Lazaro Nyalandu akiendesha moja ya Baiskeli zilizokamatwa wakati wa operesheni tokomeza.
WAZIRI wa maliasili na Utalii Lazaro Nyalandu akishuka kwenye Ndege katika uwanja wa Ndege mjini Masasi wakati wa ziara yake ya kukagua shughuli mbalimbali zinazofanywa na idara ya wanyamapori.
Nyalandu alipokuwa akikagua vipande vya meno ya tembo kwenye ofisi za idara ya wanyamapori wilayani Masasi hii leo wakati wa ziara yake.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD