TANGAZO
NA FATUMA MAUMBA, RUANGWA
MKURUGENZI wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, mkoani
Lindi,Nicolaus Kombe,amewataka watendaji na watoa huduma
wilayani humo kuhakikisha huduma muhimu za matibabu hasa dawa zinapatikana kwa
muda wote ili kuboresha huduma wilayani humo.
Aliyasema hayo katika kijiji cha Ng’au, Kata ya Mnacho,wakati wa
uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya bima ya afya ya uhamasishaji wananchi
kujiunga na mfuko wa afya ya jamii CHF unaofanywa na mfuko wa taifa wa bima ya
afya.
Kombe, amesema serikali kupitia mifuko ya
uchangiaji ya bima ya afya (NHIF) na mfuko wa afya ya jamii (CHF) imetoa fursa
kwa wamiliki wa vituo vya matibabu na watoa huduma kutumia fedha za uchangiaji
huduma kwa ajili ya ununuzi wa dawa na vitendanishi kwa ajili ya kuboresha
huduma kwa wananchi na kwamba fedha hizo sio za kulipana posho katika vikao.
Ameomba ushirikiano wa wananchi kwa ujumla
kwani mafanikio ya utekelezaji wa huduma za mfuko huo zinategemea ushiriki wa
wananchi katika kuchangia na kusimamia huduma.
“Serikali ilipitisha sera ya mabadiliko
katika sekta ya afya lengo la kuboresha huduma za matibabu na kutoa madaraka
kwa jami kupanga, kusimamia na kutoa maamuzi kuhusu huduma zinazoihusu jamii
kwani jamii ndio wamiliki wa huduma za matibabu.
“Hivyo ni muhimu tuwafahamu wawakilishi
wetu wanaosimamia huduma na niaba yetu tukishawafahamu tuwape ushirikiano na
inapobidi tuwaulize maswali kweny maeneo tunayoona hayaendi vizuri.
“Tujiunge na CHF kwa sababu sote tunafahamu
hali zetu za kiuchumi, kwa kawaida kipato chetu hakitupi nafasi ya kuweka akiba
kwa ajili ya matibabu, kila tunachopata kinaishia kwenye matumizi mengine ya
kila siku ili tuendelee kuishi, lakini ugonjwa unapoingia ghafla katika
familia, tunaanza kuhangaika kutafuta fedha za matibabu ila
ukijiunga na CHF unachangia mara moja na unapata huduma mwaka mzima.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD