TANGAZO
Na
Clarence Chilumba,Masasi.
Mbio
za mwenge wa uhuru kwa mwaka 2015 zimeingia siku ya pili mkoani Mtwara kwa
kukimbizwa wilayani Masasi huku ukianzia katika halmashauri ya mji wa Masasi
kwa kukagua miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa na serikali kwa
kushirikiana na halmashauri,wananchi pamoja na wahisani.
Akizungumza
jana wakati anatoa ujumbe wa mbio za mwenge katika viwanja vya terminal two
mjini Masasi kiongozi wa mbio za mwenge wa uhuru Juma Chumu alisema mwenge wa
uhuru una historia kubwa kwa watanzania na kwamba unapaswa kuheshimiwa na kila
mmoja ili kudumisha amani na mshikamano uliopo.
Alisema
mwenge ndio kitu pekee kinachotuunganisha hivyo ni vyema watanzania wakaulinda
umoja wetu na kwamba ukweli ni kwamba mwenge wa uhuru haukuletwa kwa ajili ya
chama,dini wala kabila fulani nchini kama wanavyosambaza uongo baadhi ya
watanzania wasioitakia mema nchi yetu.
Chumu
alisema mbio za mwenge ni chachu ya maendeleo na kwamba kila mwaka hutumika
katika shughuli za kuzindua pamoja na kuiwekea mawe ya msingi miradi mbalimbali
ya maendeleo.
Kwa
mujibu wa kiongozi huyo wa mbio za mwenge kitaifa alisema amani na mshikamano
uliopo nchini inatokana na uwepo wa alama za taifa mwenge wa uhuru ukiwemo na
kwamba Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizochangia kupatikana kwa uhuru wa nchi
mbalimbali zilizotuzunguka.
Akizungumzia
kuhusu rushwa Chumu alisema rushwa ni adui wa haki inayochangia kwa kiasi
kikubwa kupatikana kwa viongozi mafisadi na wala rushwa ambao hugombea nafasi
hizo kwa lengo la kujitajirisha na si kwa ajili ya kuleta maendeleo ya wananachi.
“Wananchi
wa Masasi nawaasa mjitokeze kwa wingi kujiandikisha kama ujumbe wa mwenge wa
mwaka huu unavkupatikana kwa viongozi mafisadi na wala rushwa ambao hugombea
nafasi hizo kwa lengo la kujitajirisha na si kwa ajili ya kuleta maendeleo ya
wananchi.
“Wananchi
wa Masasi nawaasa mjitokeze kwa wingi kujiandikisha kama ujumbe wa mwenge wa
mwaka huu unavyosisitiza ili muweze kupata sifa za kupiga kura pamoja na
kuipigia kura ya ndio au hapana katiba inayopendekezwa…hivyo fursa yenu ya
kipekee kwa sasa ya kupata viongozi bora ni kujiandikisha”.alisema.
Mbio
za mwenge wa uhuru wilayani Masasi zimekimbizwa kwa umbali wa kilometa 75 na
kupita kwenye tarafa mbili,kata tano na vijiji 17 ambapo jumla ya miradi 8 imepitiwa
na mbio hizo huku miradi miwili ikifunguliwa,mitatu imekaguliwa na mitatu imezinduliwa
yenye jumla ya shilingi bilioni 2.9.
Katika
halmashauri ya mji wa Masasi jumla ya miradi mitatu ilizinduliwa ikiwemo nyumba
ya mkurugenzi wa halmashauri ya mji,shule ya MacDonald English Medium pamoja na
ghala la kuhifadhia mazao la mama Kate Kamba.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD