TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Masasi.
MTANDAO wa polisi wanawake Tanzania wilaya ya
Masasi mkoani Mtwara wametoa misaada mbalimbali ya chakula kwa watoto wenye ulemavu
wa ngozi katika shule ya msingi Masasi halmashauri ya mji wa Masasi.
Mtandao huo ulifanya ziara shuleni hapo kwa
ajili ya kutoa msaada huo pamoja na kuzungumza na watoto hao ikiwa kama sehemu
moja wapo ya kazi za mtandao huo wilayani hapa.
Misaada iliyotolewa na kukabidhiwa kwa
wanafunzi hao wenye ulemavu wa ngozi ni pamoja na mchele kilogramu 20, Mafuta
ya kula lita 10, sukari kilogramu 20, majani ya chai katoni moja pamoja na
fedha taslimu shilingi 45,000.
Akikabidhi msaada huo hii leo kamanda wa polisi
mkoa wa Lindi ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mtandao wa polisi
wa kike Tanzania Renatha Mzinga alisema jeshi la polisi liko kwa ajili ya
kulinda haki za watoto nchini wakiwemo watoto wenye ulemavu wa ngozi.
Alisema kwa sasa baadhi ya wananchi wenye tamaa
ya fedha wamekuwa wakiwaua na kukata viungo vyao watu wenye ulemavu wa ngozi
kwa madai ya kujipatia utajiri au nafasi kubwa katika uongozi ambapo alisema
jeshi la polisi nchini limekuwa likipambana na watu hao kwa kuhakikisha
wanafikishwa kwenye vyombo vya sheria.
Mzinga alisema jukumu la mtandao wa polisi wa
kike Tanzania ni pamoja na kulinda maisha ya watoto wenye ulemavu wa ngozi ili
watu wenye lengo mbaya na kundi hilo wakamatwe na wafikishwe mahakamani.
Kwa upande wao wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi
wa shule ya msingi Masasi Samson Charles (17) na Agnes Robert (13) walisema
wanapatwa na uchungu mkubwa pale wanaposikia au kuona kwenye vyombo vya habari
kuwa baadhi ya wenzao wenye ulemavu wa ngozi wamekuwa wakiuawa kwa madai kuwa
ngozi yao ni thamani.
Waliliomba jeshi la polisi nchini kuwapa ulinzi
wa kutosha katika mazingira wanayoishi ikwa kuwa na wao wanastahili kuishi kama
ilivyo kwa watoto wengine nchini.
MWANAFUNZI mwenye ulemavu wa ngozi Samson Charles anayesoma katika shule ya msingi ya Masasi halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara akipokea ndoo ya mafuta lita 10 kutoka kwa kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga hii leo.
MWANAFUNZI Samson Charles akikabidhiwa mchele kilogramu 20 kutoka kwa kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga.
AKIMKABIDHI pakiti ya majani ya chai
Kamanda wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga Akikabidhi fedha taslimu kiasi cha shilingi 45,000/= kwa wanafunzi wa shule ya watoto wenye ulemavu halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara.
BAADHI ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi na macho wa shule ya msingi Masasi iliyopo Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara wakiwa wamekaa kwa pamoja shuleni hapo.
OFISA mnadhimu wa jeshi la polisi mkoa wa Mtwara George Salala wakati akiongea na walimu pamoja na wanafunzi wa shule ya walemavu wa ngozi na macho ya Masasi wakati wa kutoa msaada huo kwa watoto hao hii leo walipotembelea shuleni hapo.
MWANAFUNZI Samson Charles akiwa ameshikilia mfuko wa kilo 20 uliokuwa na sukari baada ya kukabidhiwa kutoka kwa mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga.
MWENYEKITI wa mtandao wa polisi wa kike Tanzania mkoa wa Mtwara TPF-NET Mariamu Emanuel Masalu akizungumza wakati wa kukabidhi zawadi kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi ya Masasi.
MWANAFUNZI mwenye ulemavu wa ngozi Samson Charles (17) anayesoma darasa la saba katika shule ya Msingi Masasi mkazi wa kijiji cha Magumuchila halmashauri ya mji wa Masasi wakati anazungumza na waandishi wa Habari hii leo ambapo alisema anashikwa na uchungu pale anaposikia kuwa watu wenye uleamavu wa ngozi kama yeye wanauawa.
Agness Robert (13) anayesoma darasa la sita shule ya msingi Masasi mkazi wa Dar es salaam nae alipata fursa ya kuzungumza na wanahabari waliofika shuleni hapo hii leo.
BAADHI ya wanafunzi wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi Masasi wakiwa kwenye picha ya pamoja.
MWALIMU Millanzi wa shule ya msingi Masasi ya watoto wenye ulemavu wa ngozi akiwaongoza wanafunzi wa shule hiyo kuimba wimbo maalumu kwa wageni waliotembelea shuleni hapo.
MWENYEKITI wa Mtandao wa polisi wa kike Tanzania wilaya ya Masasi Halima Saidi akikabidhi ndoo ya mafuta kwa mwanafunzi Samson Charles mwenye ulemavu wa ngozi.
KAMANDA wa polisi mkoa wa Lindi Renatha Mzinga akizungumza na watoto wenye ulemavu wa ngozi wa shule ya msingi Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD