TANGAZO
Tarbenaculo liko nyuma ya Pazia kwenye maandishi mekundu |
Na
Clarence Chilumba,Ruangwa.
Watu watano
wanaodhaniwa kuwa ni majambazi wamevamia na kuvunja madirisha katika kanisa
katoliki la matakatifu Joseph Mfanyakazi parokia ya Malolo jimbo la Lindi na
kufanikiwa kuiba kifaa kinachotumika kuhifadhia ekaristi takatifu (TABERNACULO)
kwa madai kuwa kifaa hicho kimetengenezwa kwa kutumia dhahabu.
Tukio
hilo la kushangaza ambalo limewaacha waumini wa kanisa hilo wasijue cha kufanya
limetokea Alhamisi April 16 mwaka huu
majira ya saa 8:30 usiku ambapo watu hao
walivamia na kuvunja baadhi ya madirisha ya kanisa hilo lenye historia kubwa nchini
lililojengwa mwaka 1939.
Akithibitisha
kutokea kwa tukio hilo paroko wa kanisa katoliki parokia ya Malolo,Theophan
Membe alisema siku ya tukio hakuwepo kanisani hapo na kwamba alikuwa safarini
jimboni Lindi kuhudhuria misa takatifu ya mapadre wa jimbo la Lindi iliyoongozwa na Askofu wa jimbo hilo Mhashamu
Bruno Ngonyani.
Alisema
alirejea parokiani hapo siku ya ijumaa ambapo wakati anasalimiana na mpishi
wake alimpa taarifa hizo kuwa kanisa limevunjwa madirisha na watu wasiofahamika
na Tarbenaculo limeibiwa na kwamba hawajui ni nani amehusika na tukio hilo ambalo
amekiri tangu aanze kufanya kazi ya upadre hajawahi kusikia hata kuona kifaa
hicho kikiibiwa.
“Tukio
hili limenisikitisha sana kwani tangia nianze kufanya kazi hii ya upadre haijawahi
kutokea… huu ni ujinga kwa waliohusika na wizi huo kwani najua wanadhani kuwa
kifaa kile kimetengenezwa kwa dhahabu nasikitika sana kizazi hiki cha Dijitali
kuwa na mawazo ya kijinga namna hii…kama mungu anasikia kilio change naomba
watu hawa walaaniwe”.alisema Membe kwa uchungu.
Alisema
baada ya kushuhudia kuwa ni kweli alimpa taarifa mwenyekiti wa kigango cha
Malolo Cleophas Nnonjela kuhusu tukio hilo na kwamba siku ya jumamosi walitoa
taarifa kituo cha polisi Ruangwa kilichomtaka mwenyekiti huyo kwenda na
katekista wa kigango hicho Moris Nguli.
Kwa
mujibu wa Padre huyo alisema parokia ya Malolo ni miongoni mwa parokia
zilizotoa wasomi wengi mkoani Lindi kutokana na historia yake ya kuingia mapema
kwa wamisionari waliongia kijijini hapo mwanzoni mwa miaka 1890 na kufanikiwa
kujenga shule ambayo imetoa maprofesa akiwemo profesa Max Mmuya,marehemu
Dkt.David Mwambe na viongozi kadhaa waliowahi kushika nyadhifa mbalimbali
nchini.
Alisema
kwa kwa mujibu wa sheria za Roma za kanisa hilo mahali ambapo Tarbenaculo
huibiwa ukristo hufa kwa muda mpaka pale wahusika hao walioiba kifaa hicho
watakapokiri kuwa ni kweli wameiba mbele ya waumini wa kanisa hilo ndipo askofu
wa jimbo hilo atakapoondoa dhambi hiyo ya mauti kutoka kwa waumini kwenda kwa
wezi hao ambao amekiri kuwa ni dhahiri adhabu ya moto inawasubiri.
Huduma
ambazo hazitakuwepo kwa sasa kwa waumini wa kigango hicho ni pamoja na ibada ya
jumapili,misa ya kila siku asubuhi,misa ya katekista,upigwaji wa kengele
zinazoashiria masaa kwa waumini hao ikwemo majira ya saa 12:00 asubuhi,saa sita
mchana na saa 12:00 jioni pia nazo hazitakuwepo.
Alisema
katika kipindi hicho pia huduma kama za ubatizo,kipaimara,komunio
takatifu,kitubio,misa za mazishi,mpako kwa wagonjwa,sherehe za ndoa pamoja na
masuala yote ya msingi yanayohusu kanisa katoliki huku akikiri kuwa waumini wa
vigango vitatu vilivyobaki wataendelea kupata huduama hizo kama kawaida.
“Binafsi
ninachosubiri kwa sasa ni muongozo kutoka kwa baba askofu juu ya hatima ya
suala hili…jana nimeongea na makamu wa askofu baba Angelus Chitanda ambaye alinitaka nisubiri mwongozo lakini
kiimani ya dhehebu letu la katoliki hapa hakuna ukristo tena mapaka pale wezi
watakapopatikana na kukiri mbele ya waumini kinyume na hapo ukristo unakufa
mahali ambapo ni chimbuko la parokia ya Malolo”. Alisema Membe.
Katika
hatua nyingine watu wasiofahamika walivamia na kufanikiwa kuvunja mlango wa
nyumba anayoishi padre huyo parokiani hapo usiku wa jumapili ya wiki hiyo hiyo
lilipotokea tukio la wizi wa Tarbenaculo ambapo hawakufanikiwa kuiba chochote
kutokana na mpishi wa padre huyo ambaye alilala ndani ya nyumba hiyo kuamka na
wezi hao kutokomea kusikojulikana.
“Sijui
ni nini nimewakosea waumini wa kigango hiki cha Malolo…mpaka wanafikia
kunifanyia vitendo vya kinyama kama hivi ambavyo haviendani na maadili ya dini
ya kikristo nadhani hapa kuna ajenda ya siri waliyonayo watu hawa hivyo ni
vyema waiweke wazi”.alisema Membe aliyeonekana kukerwa na vitendo hivyo.
Kifaa ambacho hutumika katika kuhifadhi "EKARISTI TAKATIFU" ambacho kwa nje huonekana kama kimetenegenezwa kwa kutumia DHAHABU wakati si kweli mazingira ambayo vijana hudhani ni Dili.
PAROKO wa kanisa katoliki parokia ya Malolo padre THEOPHANI MEMBE ambaye ameonesha kukerwa na kitendo kilichofanywa na Watu hao ambao mpaka sasa hawajulikani huku akiahidi kusitisha huduma ya ibada kwenye kigango hicho.
KANISA Takatifu la Mtakatifu JOSEPH MFANYAKAZI Parokia ya Malolo Jimbo la Lindi katika mkoa wa Lindi ambamo TARBENACULO hilo limeibiwa na watu wasiofahamika usiku wa kuamkia April 17, 2015.KANISA hilo limejengwa mwaka 1939.
NYUMBA anayoishi Paroko wa parokia ya Malolo Fr.Theophan Membe ambayo Mlango wake kwa huko nyuma umevunjwa na watu wasiofahamika waliokuwa na lengo la kuiba.
ASKOFU wa Jimbo la Lindi Mhashamu BRUNO NGONYANI ambaye anasubiriwa kutangaza adhabu kwa waumini wa kanisa katoliki kigango cha Malolo wakati wowote kutoka sasa mpaka pale waliohusika watakapokiri mbele ya waumini.
KIFAA hiko alichoshika PADRE Rangi yake hufanana na hiyo TARBENACULO ambacho vijana wengi wa kanisa hilo hudhani kuwa ni DHAHABU.
SHULE ya Msingi Malolo Halmashauri ya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ambayo iko jirani na kanisa lililoibiwa kifaa hicho cha kuhifadhia Ekaristi Takatifu.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD