TANGAZO
Waandishi
wasaidizi,wataalamu wa BVR KIT pamoja na wataalamu wa TEHAMA Halmashauri ya mji
wa Masasi mkoani Mtwara wametakiwa kufanya kazi hiyo kwa weledi mkubwa ili kuepusha
migogoro inayoweza kujitokeza katika zoezi la uborshaji wa daftari la kudumu la
wapiga kura linalotarajia kuanza April 24,2015.
Rai hiyo
imetolewa jana na kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi Mzenga
Twalibu wakati anafungua mafunzo ya siku mbili kwa waandishi wasaidizi wa
uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Alisema
suala kazi ya uboreshaji wa daftari hiyo ni nyeti hivyo wanapaswa kuzingania
maadili katika utendaji wa kazi hiyo ili wananchi wapate fursa ya kushiriki
kwenye uchaguzi mkuu ujao pamoja na zoezi la kuipigia kura ya ndiyo au hapana
katiba inayopendekezwa.
Kwa
mujibu wa Mzenga alisema ofisi ya mkurugenzi imewaamini na ndio maana wakapewa
kazi hiyo kulingana na vigezo vilivyowekwa wakati wa kutangazwa kwa kazi hiyo
nyeti kwa maslahi ya taifa kwa vizazi vya sasa na vile vijavyo.
“Mmeteuliwa
kuwa miongoni mwa watakaofanya kazi hii muhimu kwa taifa…hatutegemei kuwa mmoja
wenu atafanya ndivyo sivyo pale zoezi hili litakapoanza ambapo ukweli ni kwamba
kwa Yule atakayeharibu kazi hii atachukuliwa hatua kali za kisheria na ndio
maana kabla ya zoezi hili halijaanza ni lazima mle kiapo”.alisema Mzenga.
Alisema
zoezi hilo linafuatiliwa kwa karibu na wadau mbalimbali nchini wakiwemo
viongozi wa vyama vya siasa,waangalizi wa ndani wa uchaguzi,mashirika yasiyo ya
kiserikali pamoja na wadau wengine hivyo ni wajibu wao watekeleze majukumu yao
kwa ufanisi mkubwa.
Mafunzo
hayo ya siku mbili yameanza jana na yanatarajiwa kukamilika kseho ambapo jumla
ya washiriki 210 watapatiwa mafunzo hayo yatakayowawezesha kuandikisha wananchi
kwenye zoezi la uboreshajiwa daftari la kudumu la wapiga kura.
Mwisho.
Ofisa Uchaguzi wa Halmashauri ya mji wa Masasi mkoani Mtwara SHAIBU MWAKATIKA(Kushoto) wakati anatoa maelekezo ya namna ya utumiaji wa mashine za BVR kwa maofisa uchaguzi wa ngazi ya Kata hii leo wakati wa mafunzo ya siku mbili kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Masasi.
Hakimu wa mahakama ya wilaya ya Masasi HALFANI ULAYA akiwaapisha waandikishaji wa zoezi la daftari la kudumu la wapiga kura kwenye ukumbi wa shule ya sekondari ya wasichana ya Masasi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD