TANGAZO
Aliyekuwa Rais wa Misri Mohammed Mosri |
Makahama nchini Misri imemuhukumu
aliyekuwa rais wa zamani Mohammed Mosri kifungo cha miaka 20 gerezani kutokana
na kuuawa kwa waamdamanaji wakati akiwa madarakani.
Hii ndiyo hukumu ya kwanza
kutolewa kwa Morsi tangu aondolewe madarakani na jeshi la nchi hiyo mwaka 2013
kufuatia maandamano makubwa mitaani ya kupinga uongozi wake.
Yeye pamoja na viongozi wengine
wa Muslim Brotherhood walilaumiwa kwa kuwachochea wafuasi wao kumuua mwandishi
wa habari na waandamanaji wa upinzani wakati wa makabiliano nje ya ikulu ya
rais mwishoni mwa mwaka 2012.
Wakati umati ulipokusanyika nje
ya Ikulu, Morsi aliwaamrisha polisi kuwatawanya lakini wakakataa kufanya hivyo.
Baadaye Muslim Brotherhood waliwaleta wafuasi wao ambapo watu 11 waliuawa
kwenye makabiliano, wengi kutoka Muslim Brotherhood.
Kabla ya kutolewa hukumu ya leo,
Muslim Brotherhood walimlaumu rais wa sasa Abdul Fatta al-Sisi kwa kutumia
mahakama kama silaha kuhalalisha utawala wake kwa kumkandamiza Morsi. Mara
baada ya hukumu hiyo, chama cha Muslim Brotherhood kimeitisha maandamano kote
nchini humo hali iliyosababisha makabiliano makali na polisi.
Kwa mujibu wa mahakama hiyo,
rufaa ya hukumu hiyo iko wazi na mshitakiwa anaweza kufanya hivyo. Mohammed
Morsi ndiye rais wa kwanza katika Taifa hilo kuchaguliwa kwa njia ya
kidemokrasia baada ya kuangushwa utawala wa muda mrefu wa Hosni Mubarak na
waandamanaji, lakini ulidumu kwa mwaka mmoja tu kabla ya kuangushwa na jeshi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD