TANGAZO
Abdallah Ulega Mkuu wa wilaya ya Kilwa. |
Na Fatuma Maumba,
Kilwa.
Wananchi wilayani Kilwa, mkoani Lindi, wametakiwa kuona umuhimu
wa kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii CHF, ili waweze kutibiwa kwa uraisi pindi
wanapougua.
Wito huo umetolewa na Mkuu wa Wilaya hiyo, Abdallah Ulega,
kwenye uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya uhamasishaji wananchi kujiunga na Mfuko wa afya ya jamii CHF, inayofanywa na
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya katika Halmashauri kumi nchi nzima iliyozinduliwa
Kaya ya Tingi Njia nne wilayani Kilwa.
Ulega alisema sababu
inayopelekea wilaya hiyo kuwa ya
mwisho katika kujiunga na mfuko wa Afya ya Jamii
CHF, inatokana na wengi
wa kutoelewa faida na manufaa yake kama
mfuko huo umewasaidia watu wengi nchini, huku akiwataka wananchi kujiunga kwa
wingi mara baada ya kupata elimu kutoka kwa maofisa wa Mfuko wa Bima ya Afya.
“Sisi hapa Kilwa ni wa Mwisho sasa mimi sifurahii kuwa wa mwisho
nataka nihakikishe kwamba tunatoka katika nafasi ya mwisho tunaenda kuwa wa
kwanza kwani takwimu zinaonesha katika Wilaya yetu ya Kilwa takribani kaya 648 tu ndizo zilizojiunga na mfuko wa afya ya
jamii(CHF) ambayo ni sawa na asilimia 2.2 tu ya kaya zote.
“Sasa nawaombeni Leo wote mliokuwepo hapa hakikisheni mnajiunga
Na CHF, wenzetu Nachingwea wao wamepiga hatua kubwa zaidi kwani Kaya
zilizojiunga kwao ni kaya 3,009 ambayo ni sawa na asilimia 15 ya kaya zote
zilizopo Nachingwea…Idadi hii ya kaya 648 hapa Kilwa ni ndogo sana jitihada za
makusudi lazima zifanyike ili kubadilisha.
Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya hiyo alisema kutokana na idadi
ndogo za kaya zilizojiunga katika wilaya yake angependa idadi hiyo ifikie
asilimia angalau 15 ifikapo juni 2016“Ninawahimiza Bima ya afya mkoa na Ofisi
ya Mkurugenzi kukaa na kuibua mikakati ya pamoja ili tutoke hapa tulipo na ningependa
pia kupata taarifa kila baada ya miezi mitatu kuona tunaendeleaje.
Mkurugenzi wa Masoko na utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya,
Athumani Rehani, alisema katika mkoa wa Lindi utekelezaji wake bado uko chini
hasa wilaya ya Kilwa, kutokana na Kaya zilizojiandikisha kuwa ni chache ukilinganisha na idadi kubwa ya watu waliopo katika
wilaya hiyo.
Alisema katika kuhakikisha wananchi wanajiunga na
huduma za mfuko wa afya ya jamii (CHF) mfuko huo wanapita Kata 10 kati ya kaya
21 za wilaya ya Kilwa kuhamasisha wananchi kuona umuhimu wa kujiunga na huduma
hiyo.
Pamoja na mambo mengine Mfuko huo WA Taifa WA Bima ya Afya,
katika uzinduzi huo wametoa mashuka 150 kwa ajili ya hospitali na vituo
vichache vya afya vilivyopo katika wilaya hiyo ya Kilwa huku wakitoa huduma ya
upimaji bure ya magonjwa yasiyoambukiza kwa wakazi
waliojitokeza kwenye uzinduzi huo.
Mwisho.
Mkuu wa wilaya
ya Kilwa, Abdallah Ulega akizungumza na Wananchi wa Kijiji cha Njia Nne, Kata
ya Tingi wilayani Kilwa, wakati wa uzinduzi wa awamu ya pili ya kampeni ya
uhamasishaji kwa wananchi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii (CHF) inayofanywa na
Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) katika Halmashauri kumi nchini.
Mkuu wa wilaya ya
Kilwa, Abdallah Ulega (kushoto) akipokea sehemu ya mashuka 150 kutoka kwa
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani
Athumani(kulia) kwa ajili ya Zahanati za Wilaya ya Kilwa.
Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti
wa Mfuko wa Bima ya Afya (NHIF), Rehani Athumani akielezea namna kampeni
hiyo inavyofanyika katika halmashauri nyingine kumi na hivyo kufanya jumla ya
halmashauri zilizohamasishwa nchi nzima kufikia halmashauri 74 katika mwaka wa
fedha wa 2014/15, katika uzinduzi uliofanyika katika Kijiji cha Njia Nne,
Kata ya Tingi wilaya ya Kilwa, Mkoani Lindi.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD