TANGAZO
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
OFISI YA
WAZIRI MKUU
TAWALA
ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
HALMASHAURI YA MJI MASASI
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RATIBA YA ZOEZI LA UANDIKISHAJI KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA
WAPIGA KURA KWA KUTUMIA MFUMO WA KIELEKTRONIKI WA BVR KWA HALMASHAURI YA MJI WA
MASASI.
Ndugu Wananchi, kama tunavyofahamu
kwa sasa nchi yetu iko kwenye zoezi nyeti la uboreshaji wa daftari la kudumu la
wapiga kura kwa kutumia mfumo wa kuchukua taarifa za mwili au tabia ya
mwanadamu na kuzihifadhi kwa ajili ya matumizi.(Biometric Registration).
Zoezi hili ni la kawaida ambalo tume
ta Taifa ya uchaguzi imeamua kufanya marekebisho ya taarifa za wapiga kura
kwenye daftari la wapiga kura litakalotumika wakati wa uchaguzi.
Ndugu wananchi, Watakaoandikishwa ni
wananchi wote waliowahi kuandikishwa hapo awali, waliotimiza umri wa miaka 18
na kuendelea na wote ambao kwa sababu mbalimbali hawakuwahi kuandikishwa ikiwa
ni pamoja na wale watakaotimiza umri wa miaka 18 ifikapo siku ya uchaguzi, yaani Oktoba 2015.
Halmashauri
ya mji wa Masasi ni miongoni mwa Halmashauri saba (7) mkoani Mtwara yenye kata
14 ambapo jumla ya wananchi 83,798 wanatarajiwa kuandikishwa kwenye zoezi la uboreshaji
wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Ndugu
wananchi, Zoezi hili kwa Halmashauri ya Mji wa Masasi lilianza jumatatu
April 24, mwaka huu katika kata za Mtandi, Jida, Chanikanguo pamoja na Mkuti na
ambalo bado linaendelea hadi sasa ambapo kwa kata hiyo litakamilika tarehe
30/04/2015 saa 12:00 Jioni.
Kwa ujumla uandikishaji katika Halmashauri ya mji wa Masasi utadumu
kwa muda wa siku ishirini na nane (28) ili kuwezesha wananchi wote wa mji wa
Masasi kuweza kujiandikisha kwa wingi waweze kupata sifa za kushiriki kwenye
uchaguzi mkuu ujao pamoja na zoezi la kuipigia kura ya ndio au hapana katiba
inayopendekezwa.
Ndugu Wananchi kuanzia tarehe 02/
hadi 08/05/2015 zoezi la uandikishaji litaendelea kwa kata zingine nne za Nyasa,Napupa,Marika
pamoja na Mumbaka ambapo kila mwananchi wa kata hizo anapaswa kwenda
kujiandikisha kwenye kituo chake kilichopo kwenye mtaa wake anaoishi.
Tarehe 10 hadi 16/05/2015 kata
zitakazohusika kwenye zoezi hilo la uandikshaji ni pamoja na kata
za Mkomaindo,Migongo na Temeke na kata zitakazokamilisha zoezi hili ni
kata za Mwenge Mtapika,Sululu na Mwenge ambazo zoezi la uandikishaji litaanza
tarehe 18 hadi 24/05/2015.
Ndugu Wananchi Vituo vya
kujiandikisha kila siku vitafunguliwa saa 2:00 Asubuhi na vitafungwa saa 12:00
Jioni kwenye kata zote zilizopo Halmashauri ya Mji wa Masasi.
“Nitoe wito kwa wananchi wa mji
wa Masasi kujitokeza kwa wingi kushiriki kwenye zoezi hili muhimu kwao na kwa
Taifa…wawahi kufika kwenye vituo vyao ambavyo kila mtaa kuna kituo kimoja cha
kujiandikisha ambacho wananchi wa eneo husika wanapaswa kwenda kujiandikisha,pia
nitoe rai kuwa wananchi wasisubiri hadi siku za mwisho ndipo waende
kujiandikisha”.
“Natoa wito pia kwa waandikishaji
pamoja na wataalamu wa mashine za BVR watambue kuwa wameteuliwa kuwa miongoni mwa watu
watakaofanya kazi hii muhimu kwa taifa…
Hivyo mnatakiwa kuwa makini kutimia wajibu na majukumu yenu ya kila siku ili
kufanikisha mchakato wa uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
Hatutegemei kuwa mmoja wenu
atafanya ndivyo sivyo wakati wote wa zoezi hili na kwamba ukweli ni kwamba kwa
Yule atakayeharibu kazi hii atachukuliwa hatua kali za kisheria na ndio maana
kabla ya zoezi hili kuanza mliapa”.
Aidha, Natoa wito kwa wanasiasa, kama ilivyokuwa
katika utaratibu wa zamani, Wawakilishi wa Vyama vya Siasa wataruhusiwa kuwepo
katika vituo vya kuandikisha Wapiga Kura.
Jambo hili ni muhimu kwani linasaidia kudhihirisha uwazi katika zoezi
zima. Wajibu wa Wawakilishi wa Vyama vya
Siasa kama ilivyoelezwa ni kuangalia kwamba Sheria, Kanuni, na Taratibu
zilizowekwa na Tume zinazingatiwa katika uandikishaji.
“Ni vyema ieleweke kwamba hawatakiwi kuwaingilia waandishi wasaidizi na wataaalamu wa
BVR wanapotekeleza wajibu wao”.
Kwa ujumla zoezi la uandikishaji hadi sasa ndani ya
Halmashauri yetu ya mji wa Masasi linaendelea vizuri licha ya kuwepo kwa baadhi ya changamoto chache zinajitokeza
kwenye vitu vya kujiandikisha ambazo
nyingi zimekuwa zikipatiwa ufumbuzi wa
haraka kutoka kwa wataalamu wa mifumo kwa ngazi ya halmashauri ya mji wa Masasi
kwa ushirikiano na wale wa kutoka tume ya Taifa ya uchaguzi.
Mwisho:
Naomba kutoa wito
kwa wananchi wote walio na sifa
ya kuwa Wapiga Kura kwa Halmashauri ya Mji wa Masasi wajitokeze kwa wingi ili wajiandikishe. Aidha napenda kuwahakikishia kuwa Halmashauri ya Mji wa Masasi kwa
kushirikiana na Serikali wilayani hapa imedhamiria kuhakikisha
kuwa zoezi hili linafanyika kwa amani na ufanisi mkubwa.
Ahsanteni Sana Kwa Kunisikiliza:
IMETOLEWA NA:
..................................
FORTUNATUS KAGORO
MKURUGENZI HALMASHAURI YA MJI
WA MASASI.
APRIL 28,2015.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD