TANGAZO
VITUO VITAKAVYOTUMIKA KUANDIKISHA WAPIGA KURA KATIKA DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA KWA KATA ZA NYASA, NAPUPA, MUMBAKA NA MARIKA KUANZIA TAREHE 02 HADI 08/05/2015. |
MLUNDELUNDE:
Vituo ni Mpota
Ofisi ya Kitongoji, Mlundelunde Ghalani, Mlundelunde Shuleni na Mchaka Ofisi ya
Kitongoji.
NAMIKUNDA:
Vituo vitakuwa
Namikunda Shuleni, na Namikunda Ghalani.
CHIPOLE:
Vituo ni Chipole
Ghalani pamoja na Chipole Shuleni.
MUMBAKA:
Vituo
vitakavyotumika ni Mumbaka Zahanati na Mumbaka Ofisi ya Kata.
KATA YA NYASA:
Mtaa wa Nyasa
Ofisini kituo kitakuwa Ghalani, Nyasa Chini kituo ni Shule ya Msingi Nyasa,Mtaa
wa Nyasa A kituo ni Ofisi ya Kata,Maendeleo kituo kitakuwa katika shule ya
Msingi Maendeleo,Matankini Kwenye Nyumba za Bodi ya Korosho,Mtaa wa Nyasa B
kituo kitakuwa eneo la Gogo Vivu na Mtaa wa Mchema kituo kitakuwa nyumbani kwa
Ustaadh Judo.
KATA YA MARIKA:
Vituo
vitakavyotumika kwa ajili ya zoezi la kujiandikisha kwenye Daftari la wapiga
kura kwa kutumia mfumo wa Kielektroniki wa BVR kwa kata ya Marika ni pamoja na
Namatumu Shuleni, Namatunu Ghalani, Ipiho –Ofisi ya Kitongoji, Marika Ghalani,
Marika Shuleni, Machombe, pamoja na Mtaa wa Nakwande ambao kituo chake kitakuwa
Ofisi ya Kitongoji.
KATA YA NAPUPA:
Kwa Upande wa
Kata ya Napupa vituo viko kwenye kila Mtaa ambapo kwa upande wa mtaa wa
Wapiwapi A Kituo kipo nyumbani kwa Mzee Lazi, Wapiwapi B Msikiti wa Answar,
Kagera Sokosela, Misufini –Kambarage, Silabu eneo la Zahanati, Napupa kituo
kitakuwa shule ya sekondari ya kutwa ya Anna Abdallah, Chiwisi mtaa wa Ghalani
na Stendi ya Newala kituo kitakuwa karibu na kanisa la Anglikana.
ANGALIZO: Kila
mwananchi anapaswa kujiandikisha kwenye kituo chake kilichopo kwenye kila mtaa
wake anaoishi,Ni kosa kujiandikisha kwenye kituo kisichokuhusu. Kwa wale ambao
kata zao bado waendelee kusubiri mpaka siku itakapofika kwa kuwa Tume ta Taifa
ya Uchaguzi imedhamiria kuandikisha watu wote.
WOTE MNAOMBWA KUJITOKEZA KUJIANDIKISHA
IMETOLEWA NA KITENGO CHA HABARI NA MAWASILIANO SERIKALINI
HALMASHAURI YA MJI WA MASASI
APRIL 30,2015.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD