TANGAZO
Na Christopher Lilai, Nachingwea.
Ufinyu wa fedha za ruzuku ya uendeshaji wa shule za msingi na
sekondari (Capitation Grant) umelalamikiwa kuwa unachangia kwa kiasi kikubwa
kudidimiza elimu, kuathiri utoaji wa taaluma na kuwabebesha mzigo wazazi
na walezi na kutofikiwa matokeo makubwa sasa (BRN)katika wilaya ya Nachingwea
mkoani Lindi.
Wakizungumza
wakati wa maadhimisho ya kilele cha juma la elimu yaliyofanyika siku ya ijumaa (iliyopita)
wilayani hapa, baadhi ya walimu wakuu na wakuu wa shule na wazazi
waliiomba serikali kupeleka fedha hizo kadiri ya mahitaji ya shule na kwa
wakati.
Carlos
Matuta, mwalimu mkuu wa shule ya msingi ya Majengo ,alisema kuwa changamoto
kubwa inatokana na ufinyu wa fedha hizo zinazotolewa kuwa chache ikilinganishwa
na kiasi kinachoidhinishwa katika bajeti.
Alibainisha
kuwa kutokana na hali hiyo inawalazimu kuwaomba wazazi na walezi kuchangia michango
mbalimbali ili kuziba mapungufu katika uendeshaji wa shule hata hivyo kasi ya
uchangiaji ni ndogo kutokana na mwamko mdogo wa jamii katika sual la elimu.
Frola
Athuman Millanzi, mwalimu wa shule ya msingi ya Nachingwea alisema kuwa ufinyu
wa fedha za kuendeshea shule unachangia utoro kwa wanafunzi ambao wazazi na
walezi hawana uwezo wa kifedha hivyo kuiomba serikali kuhakikisha inatoa
kiwango kinachotakiwa tena kwa wakati.
Alisema
kuwa licha ya ufinyu pia fedha hizo zinachelewa kupelekwa kwenye shule
husika hivyo kuwapa mzingo wakuu wa shule na walimu wakuu katika
kuendesha shule na kufikia wakati kulazimika kutumia fedha zao za mishahara
kuendesha shule .
Delfina
Chikawe akizungumza kwa niaba ya wazazi aliitaka serikali kama haina
uwezo wa kutoa hiyo ruzuku hiyo kuiondoa ili wazazi wajue kuwa jukumu hilo lipo
kwako kuliko mtindo wa sasa ambapo wanadai serikali inagharamia kumbe mzingo ni
wao.
Alisema
kuwa wazazi kwa sasa wanakabiliwa na michango ambayo haiwashirikishi tena
mikubwa na kuomba serikali iwapo inashindwa kugharamia elimu hivi
sasa wakati ambapo kwa shule ya sekondari kuna ada kidogo je hapo mwakani
ambapo elimu itakuwa bure hali itakuwaje.
Kwa
upande wake afisa elimu msingi wa halmashauri ya Nachingwea,Makwasa Bulenga
kwenye taarifa ya hali ya elimu aliyoisoma kwenye maadhimisho hayo alitja
changamoto fedha za uendeshaji ambapo alisema zimekuwa zikipungua
mwaka hadi mwaka.
Bulenga alitoa takwimu ambazo zinaonesha kuwa fedha hizo kwa miaka mitano toka mwaka 2010 hadi mwaka huu zimekuwa zinapungua toka asilimia 54 mwaka 2010 hadi asilimia 24.1 mwaka huu jambo ambalo linaathiri unedeshaji wa shule.
“Fedha
za uendeshaji wa shule kutokuja kwa wakati na mtiririko wa fedha hizi umekuwa
ukipungua kwa kila awamu suala ambali linaathiri uendeshaji wa shule”alisema
Bulenga.
Amebainisha
kuwa katika kukabili changamoto hiyo wilaya inaendelea kuhamasisha jamii
kuchangia fedha ili kufidia mwanya huu hata hivyo alikiri kuwa kasi ya
uchangiaji ni mdogo.
Alisema kuwa wilaya inawasiliana na wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa na Hazina ili mgao wa fedha za uendeshaji wa shule utolewao uendane sawa na idadi ya wananfunzi waliopo shuleni na itumwe kwa wakati.
Alisema kuwa wilaya inawasiliana na wizara ya Tawala za mikoa na serikali za mitaa na Hazina ili mgao wa fedha za uendeshaji wa shule utolewao uendane sawa na idadi ya wananfunzi waliopo shuleni na itumwe kwa wakati.
Akihutubia
kwenye maadhimisho hayo mkuu wa wilaya ya Nachingwea,Paloleth Mgema
aliwataka wadau wote wakiwemo viongozi wa kisiasa,watendaji wa
halmashauri,walimu wazazi na jamii kwa ujumla kushirikiana katika kuzielewa na
kuzifanyia kazi changamoto zilizobainika kukwaza kwa namna moja ama nyingine.
“Kutokuzielewa
vizuri na kuzitafutia ufumbuzi changamoto hizo kunaweza kusababisha kuchelewa
kuyafikia matokeo makubwa sasa (BRN) katika elimu”alisema Mgema.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD