TANGAZO
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kwenye semina hiyo. |
Na Fatuma Maumba, Lindi.
Chama cha Waandishi wa Habari za Mazingira Tanzania (JET), wametoa mafunzo ya siku moja kwa
baadhi ya waandishi wa habari kutoka mkoa
wa Lindi, juu ya kuandika na kuripoti habari za migogoro ya ardhi ili kuweza kuwasaidia
wananchi wanaodhulumiwa ardhi yao.
Wakizungumza mara baada ya kumalizika
kwa mafunzo hayo, Christopher Lilai,
Bashiru Kauchumbe pamoja na Mwanja Ibadi,walisema kupitia mafunzo hayo
yaliyotolewa na JET wamejifunza mambo mengi ambayo walikuwa hawayafahamu
ikiwemo sera ya Taifa ya ardhi ya mwaka 1995 pamoja na sheria ya ardhi namba 4 na 5 ya mwaka 1999.
walisema baada ya kupata mafunzo hayo
wataweza kuandika vizuri na kuripoti masuala yote ambayo yanahusu migogoro ya
ardhi katika mkoa wa Lindi, ambayo imekuwa ikiwasumbua wananchi wengi kwenye maeneo mbalimbali mkoani humo.
Mafunzo hayo kuhusu mambo ya uandikaji wa habari za
migogoro ya ardhi yalifadhiliwa na Chama cha Waandishi wa Habari za
Mazingira Tanzania (JET), ambapo moja ya masuala ya msingi
yaliyojadiliwa kwenye kwenye mafunzo
hayo ni kuunda umoja wa waandishi wa habari wa
mkoa wa Lindi watakaofanya kazi ya kuandika masuala ya ardhi.
Hata hivyo waandishi hao walipata mafunzo
juu ya sheria za ardhi, maadili ya
taaluma ya uandishi wa habari pamoja na namna ya kuandika habari zinazohusu
masuala ya migogoro ya ardhi.
“Tulikuwa hatufahamu Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 ambayo
imeweka kanuni za msingi zinazotawala mfumo mzima wa miliki, usimamizi na
matumizi ya ardhi nchini na kanunuzi hizo ni pamoja na kutambua kuwa ardhi
ya Tanzania ni mali ya umma na kuwa imewekwa mikononi mwa Rais kama mdhamini
kwa niaba ya raia wote lakini kupitia mafunzo haya tumeyafahamu”.
Kwa upande wake, Afisa Ufuatiliaji Tathimini za miradi ya JET, Augustino Antony, alisema wametoa mafunzo hayo kwa
waandishi wa habari ili kutambulisha mradi mpya unaoitwa “Ardhi yetu na Agenda yetu”.
Alisema la mpango huo ni kuibua migogoro ya ardhi na kuiandika ili kuwapa sauti wale ambao walikosa sehemu ya kusemea ili
mamlaka husika iweze kuchukua hatua sahihi na kila mmoja apate haki na kufaidika na rasilimali za nchi.
Mwisho.
Baadhi ya waandishi wa habari kutoka mkoa wa Lindi, wakiwa kwenye
mafunzo ya siku moja ya kufuatilia na kuripoti habari za migogoro ya ardhi katika
mkoa huo, mafunzo hayo yaliandaliwa na Chama cha Waandishi wa
Habari za MazingiraTanzania (JET).
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD