TANGAZO
Madereva wanaofanya
safari zao za mikoani pamoja na wale wanaokwenda wilayani wanaoanzia safari zao
katika mji wa Masasi mkoani Mtwara wamegoma kufanya safari hizo kwa madai kuwa
wanasubiri tamko kutoka kwa viongozi wao ambao hivi sasa wako kwenye kikao na
viongozi wa serikali kwenye stendi kuu ya mabasi ya mikoani ya Ubungo jijini
Dar es salaam.
Wakizungumza kwa nyakati
tofauti na Blog
ya Mtazamo Mpya madereva hao wamedai kuwa hawataondoa magari stendi
mpaka pale hatima ya madai yao kwa serikali yatakapotekelezwa ikiwemo suala la
kurudi shuleni kila baada ya miaka mitatu kubwa liiwa ni gharama ya shilingi 500,000
wanazotakiwa kulipia masomo hayo kwenye vyuo vya udereva nchini.
Walisema kuwa kabla ya
uamuzi huo wa serikali wao kama wadau walipaswa kushirikishwa ili nao waweze
kutoa maoni yao juu ya namna ya utekelezaji wa maagizo hayo na kwamba endapo
serikali itakubaliana na madai yao basi mgomo hautakuwepo na safari zitaendelea
kama kawaida.
“Sisi kama wadau wa suala hili tulipaswa kushirikishwa tangia mwanzo
kabla halijafika kwenye vyombo vya habari…tatizo na sisi tuna kero zetu ambazo
tunapaswa kuzifikisha kwa serikali yetu hivyo walipaswa kukaa pamoja na
viongozi wetu haya yote tunadhani yasingetokea”.
Kwa upande wao baadhi ya
abiria walioongea na Blog hii ambao hadi sasa wako stendi kuu ya mabasi ya mji
wa Masasi wamedai kuwa hawajui hatima yao hadi sasa ingawa uko uwezekano wa
kurudishwa kwenye maeneo yao walikotoka ikiwemo wilaya za wilaya Newala,Tandahimba,Nachingwea,Tunduru,Nanyumbu
pamoja na Liwale
wilaya ambazo magari ya abiria ni lazima yapite mjini Masasi.
Katika hatua nyingine
jeshi la polisi limeendelea kuimarisha ulinzi katika mji wa Masasi huku gari ya
doria yenye askari ikipita kwenye mitaa na maeneo ya stendi kuu ya Mabasi kwa
lengo la kuimarisha ulinzi wa abiria na mali zao.
Hadi Blog ya Mtazamo
mpya inaondoka katika eneo la stendi kuu ya mabasi mjini Masasi bado kulikuwa
na mazungumzo baina ya kamanda wa polisi wilaya ya Masasi Azaria Makubi pamoja na
madereva,makondakta na wakatishaji wa tiketi wa mabasi hayo lengo likiwa ni
kuwashawishi madareva hao wawarudishe abiria kule walikotoka ili kuepusha
usumbufu pamoja na gharama zinazoweza kujitokeza kwa abiria hao.
Hivi ndivyo hali ilivyokuwa asubuhi hii katika kituo kikuu cha Mabasi ya Mikoani na wiayani katika mji wa Masasi ambapo magari ya abiria yalionekana kuendelea kubaki katika eneo hilo kutokana na mgomo wa Madereva.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD