TANGAZO
Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini imekubali maombi ya chama hicho huku
ikiwataka kurudisha cheti cha usajili wa awali na kupewa cheti kingine.
Awali ACT-Wazalendo ilipata usajili kwa jina la ACT-Tanzania na baadae kuomba
kulibadili jina hilo.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Jaji
Francis Mutungi, ameridhika na maelezo yaliyokuwa yametolewa na uongozi wa
chama hicho wa sababu za kuamua kubadili jina la chama hicho kutoka
ACT-Tanzania hadi ACT-Wazalendo.
Kwa mujibu wa taarifa zilizotolewa kwa vyombo vya habari jana jiijini Dar es
Salaam, Jaji Mutungi alijibu ombi hilo kwa njia ya barua.
Katika taarifa hiyo inaeleza: "Nikurejeshe kwenye barua yenye kumbukumbua
namba AC-HQ/MSJ/2015 ya Aprili 15, mwaka 2015 ikisomwa sambamba na barua yangu
yenye kumbukumbu namba HA.322/362/20/80 ya Aprili 13, mwaka 2015 kuhusu suala
tajwa hapo juu".
Jaji Mutungi alieleza kuwa, alisoma na kuyatafakari kwa kina maelezo katika
barua ya ACT-Wazalendo, na kwamba ameridhika na maelezo yao kuhusu jina jipya
la chama hicho kwa mujibu wa kanuni ya 7 ya kanuni za usajili wa vyama vya siasa.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD