TANGAZO
Na
Clarence Chilumba,Masasi.
Paroko
wa kanisa katoliki parokia ya Masasi jimbo la Tunduru Masasi mkoani Mtwara Dominick
Mkapa amekemea vitendo vya rushwa vinavyofanywa na baadhi ya watu waliopewa
mamlaka serikalini mazingira yanayochangia kuwepo kwa mikataba mingi isiyo na
tija kwa taifa letu.
Aliyasema
hayo jana wakati anatoa mahubiri kwenye misa takatifu ya mkesha wa pasaka
ambapo alisema kila siku wananchi wamekuwa wakilalamika kwa kukosa huduma
katika maeneo mengi ikiwemo mahakamani,hospitali,vituo vya polisi kutokanana
waliopewa dhamana kudai rushwa ili watoe huduma kitu ambacho amekiri kuwa ni
dhambi.
Alisema
hakuna uhuru wa kweli pale vyombo vilivyopewa dhamana na mamlaka ya kusimamia
haki vitakapokuwa havitendi haki kwa kuwalazimisha wananchi kutoa
rushwa,kuwafanyia vitendo vya uonevu pamoja na kujigeuza wao kuwa miungu watu
kwa watu hao hao waliowapa dhamana hizo.
Alisema
ufufuko wa kristo ndio imani kuu ya ukristo na kwamba bila ufufuko wa kristo
basi hakuna imani ya maisha ya binadamu mara baada ya kifo ambapo aliwaasa
wakristo kupendana kama mwokozi wao alivyowapenda hata akakubali kufa msalabani
kwa ukombozi wa walio wanyoofu wa moyo
hata wale wenye dhambi.
Kwa
mujibu wa Mkapa alisema historia ya Tanzania inaonesha kuwa ilipata uhuru mwaka
1961 lakini hadi sasa hakuna uhuru wa kweli kutokana na baadhi ya viongozi
kufanya vile wanavyodani kuwa inafaa kuongoza kwa maslahi yao binafsi huku
kundi kubwa la watu likibaki hoi.
Alisema
huwezi kusema kuna uhuru wa kweli huku wachache waliopewa dhamana
wakijilimbikizia mali kwa faida yao na familia zao na pia huwezi kukiri uwepo
wa uhuru wa kweli huku wale walio wengi wakikosa mahitaji yao ya msingi kama
vile elimu,afya pamoja na maji safi na salama.
Aidha
paroko huyo aliwakumbusha wakristo nchini kuwa pasaka ni adhimisho la ufufuko
wa yesu kristo na kwamba wanapaswa kuendelea kutenda yaliyo mema waliyoyatenda
wakati wa kwaresma mwezi mmoja uliopita.
Alisema
wakati muafaka sasa umefika kwa viongozi waliopewa dhamana na wananchi nchini kuacha vitendo vyote vinavyokwenda kinyume na
maandiko ya vitabu vya mungu ikiwemo rushwa,ufisadi na badala yake wamrudie mungu kwa kutenda haki
mema machoni pake.
Mkapa
alisema baadhi ya viongozi waliopewa dhamana nao pia ni miongoni mwa waumini wa
dini ya kikristo hapa nchini na kwamba
nao wanapaswa kuishi kwa kufuata maisha aliyoishi mkombozi wao yesu kristo na
kwamba vitendo vya ukiukwaji wa maadili vinavyoendelea kushamiri hapa nchini ni
ishara tosha kuwa baadhi ya viongozi hao waumini wameshindwa kufuata maisha ya
yesu kristo aliyefufuka.
Wakristo
nchini wanaungana na wakristo wenzao duniani katika adhimisho la ibada ya sikukuu
ya pasaka kama kumbukumbu ya ufufuko wa bwana yesu kristo aliyeteswa na
hatimaye kufufuka miaka elfu mbili iliyopita.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD