TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara
JINAMIZI ambaye anaitesa timu ya
Ndanda FC ya mkoani Mtwara, kuendeleza kutoka sare ama kufungwa kwenye uwanja
wa nyumbani limeendelea kuwatesa na kuwaumiza mashabiki wake na
kumtaka kocha Mkuu wa timu hiyo Meja Mstaafu Abduli Mingange kuachia ngazi na
kuwapisha wengine waendelee na kazi.
Akizungumza na Blog ya Mtazamo Mpya, jana kwenye
uwanja wa Nangwanda Sijaona, shabiki wa timu hiyo Abdallah juma, alisema
kitendo cha kuendelea kufanya vibaya kwenye uwanja wa nyumbani kinawakatisha
tamaa mashabiki wa timu hiyo kwa nini imekuwa ikivulunda uwanja nyumbani
wakati wenzao uwanja wa nyumbani wanashinda.
Alisema Ndanda ina wachezaji wazuri
sana na wanapokuwa uwanjani wanacheza vizuri lakini tatizo lao
wamekuwa wakidharau timu ndogo tofauti wanapocheza na timu kubwa kamaYanga,
Simba au Azam.
“Wachezaji wa timu ya Ndanda wameshajiona
tayari wameshakuwa wachezaji bora na wenye viwango vya juu kwa sababu ukiwaangalia wanapokuwa uwanjani
wanacheza vizuri lakini wamekuwa wakishindwa kufanya vizuri lakini yote hii
inatokana na dharau ya kudharau timu ndogo…Wewe angalia wanapocheza na timu
kama Yanga, Simba au Azam wanavyokuwa makini hawataki kushindwa lakini kwa nini
wafungwe na timu hizi ndogo ndogo au watoke sare? Alihoji Juma.
Saidi Mohamedi ni shabiki wa timu ya
Ndanda Fc, yeye alimlalamikia mwalimu wa timu hiyo kwa kumtoa mchezaji
Nzuri Jacob Masawe na kumuingiza mchezaji mwingine ambaye kiwango chake si
kizuri.
“Mimi kimenikera sana kitendo cha
kocha Mkuu wa Ndanda kumtoa Jacob Masawe kipindi cha pili na kumuingiza
mchezaji mwingine wakati Masawe alikuwa na uwezo wa kucheza hadi dakika 90 zote
bila matatizo…ningekuwa na uwezo wa kuongea na uongozi wa Ndanda ningewaambia
kocha angekuwa mtu wa kwanza kujiudhuru kwa sababu anaambiwa aingize wachezaji
wazuri yeye anafanya mabadiliko kwa chuki anamtoa mchezaji mahili
Jacob Masawe kitendo hiki kimewakera mashabiki wengi si mimi pekee yangu.
Kwa upande wake Kocha Mkuu wa timu ya
Ndanda FC, Meja Mstaafu Abduli Mingange, amewalalamikia wachezaji wake kwa
nafasi walizozipata wakashindwa kuzitumia kwa kufunga magori mengi.
“Wachezaji wangu walipata nafasi
nyingi sana nzuri lakini wameshindwa kutumia mwanya huo kwa kufunga magori
mengi mimi kocha kazi yangu kuwafundisha jinsi ya kupambana uwanjani na kufunga
magori, kocha hawezi kuchukua mpira na kutumbukiza gorini nadhani hata
nyinyi wenyewe mmeona nafasi walizozipata na wameshindwa kuzitumia.
“Kiukweli wananikatisha tamaa
wachezaji wangu lakini siwezi kuwasusa kwani mtoto wako akiwa mwizi utamkataa
uwezi kumkataa utaendelea kumwelekeza mpaka hataacha wizi ndio mimi nitaendelea
kuwafundisha zaidi na zaidi…hasikuambie mtu hii Ligi ni ngumu sana kila mtu
anataka ushindi ila nitapambana hadi dakika ya mwisho kufa na kupona na
hatuwezi kushuka daraja hata siku moja, kikubwa mipango yangu ni kuendeleza
kuboresha na kuimalisha sehemu ya ufungaji wa magori kwa wachezaji wangu.
Katika mchezo uliochezwa jana katika
uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani Mtwara, timu ya Ndanda Fc walikuwa wa kwanza
kuzifumania nyavu za wapinzani wao dakika ya 14 Kigi Makasi aliipatia timu yake
bao la kwanza hadi mapumziko bao 1-0.
Lakini kipindi cha pili Mbeya City
walirudi kwa kasi kali ambapo dakika ya 76 Themy Felix akaipatia timu
yake bao la kusawazisha na mpaka mpira unamalizika Ndanda Fc moja na Mbeya City
moja.
Katika mchezo wa jana kikosi cha
Ndanda kiliongozwa na golikipa Wilbert Mweta, Azizi Sibo, Paul Ngalema, Hemed
Khoja, Kasian Ponera, Zabron Raimond, Jacob Masawe, Masoud Ally, Gideon Benson,
Nasoro Kapama na Kigi Makasi na wachezaji wa akiba ni Jeremia Kisubi, Shukuru
Chachala, Omega Seme, Ibrahim Mwaipopo, Rajabu Isihaka, Said Issa na Salumu
Minelly.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD