TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
WAKATI timu ya Ndanda Fc ikijifua kwa mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa jumamosi dhidi ya Mbeya City mkoani Mtwara, timu hiyo inakabiliwa na hali mbaya kiuchumi, huku wadau mbalimbali wakitakiwa kuichangia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuondokana na tatizo hilo.
WAKATI timu ya Ndanda Fc ikijifua kwa mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mchezo wa jumamosi dhidi ya Mbeya City mkoani Mtwara, timu hiyo inakabiliwa na hali mbaya kiuchumi, huku wadau mbalimbali wakitakiwa kuichangia timu hiyo kwa hali na mali ili iweze kuondokana na tatizo hilo.
Akizungumza na Blog ya Mtazamo Mpya,jana kwenye uwanja
wa Nangwanda Sijaona mkoani humo, Afisa Habari wa timu hiyo, Idrisa Bandali,
alisema licha ya timu yao kujiandaa vizuri na mechi hiyo ya jumamosi dhidi ya
Mbeya City, timu yao kwa sasa ina hali mbaya kiuchumi kitu ambacho kinaweza
kupelekea kufanya vibaya siku ya mechi.
“Timu yetu ina
matatizo pamoja na kujiandaa na mchezo dhidi yetu na Mbeya City April 4 mwaka
huu bado tuna matatizo ya kiuchumi ambayo pengine yanaweza yakahatarisha hata
ushiriki wetu nzuri tuna tatizo la kiuchumi linalikabili timu yetu pia kuna
tatizo sehemu ya kulala mambo ya chakula ndio tatizo kubwa.
“Ninapozungumza
sasa hivi tunatembeza barua ili kuweza kuomba misaada kwenye makampuni
mbalimbali, watu binafsi, viongozi wa serikali, wabunge watusaidie kuhakikisha
kwamba timu yetu inakaa sehemu nzuri…Kama timu tuendelee kumshukuru Waziri
wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa(TAMISEMI)Hawa
Ghasia,ambaye anaendelea kutoa posho shilingi milioni moja na laki mbili kila
wiki endi ili ni jambo la kuigwa sana kwa watu wengine, hadi sasa ameisaidia
timu jumla ya shilingi milioni kumi na saba.
Bandali alisema
kwamba kama Waziri Ghasia amewasaidia suala la posho watu wengine wawasaidie
mambo ya chakula, maradhi kimsingi yanaisababishia timu kuwa kwenye hali mbaya,
kwa mfano wao kwa siku wanatumia shilingi milioni saba na elfu 30 mambo ya
maradhi na chakula wale ambao wanawasaidia kwenye kulipa hivyo vitu milija yao
ya kutoa fedha imekuwa ngumu.
Hata hivyo Bandali
alisema anaomba wadau, wenye nia njema na timu ya Ndanda na wale wakeleketwa wa
kuisaidia timu kwani inakusudio la kubaki ligi kuu ili mwakani waweze kujipanga
vizuri kwenye msimamo unaokuja sasa watabaki vipi kama hali yao ya kiuchumi ni
mbaya wanaitaji wapate fedha hili waweze kutatua matatizo madogo madogo kwenye
timu ikiwemo wachezaji wenyewe pia kuwafanya wachezaji wawe uhuru wacheze mpira
wasifikirie kitu kingine.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD