Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

DIWANI WA CCM MTWARA ADAI HAKUOMBA NAFASI HIYO KWA LENGO LA KUJITAJIRISHA...

TANGAZO
Na Fatuma Maumba, Mtwara
DIWANI wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Kata ya Vigaeni, iliyopo Halmashauri ya Mtwara-Mikindani, Mkoani Mtwara, Saidi Nassoro, amesema kwamba yeye hajaomba Udiwani kwa sababu aje kupata riziki ameomba Udiwani ili kuja kuleta maendeleo kwa wananchi wa Kata hiyo.

Alisema hayo jana kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye Kata hiyo, na kuongeza kwamba kipindi anaanza Udiwani katika Kata yake alikuta kuna vikundi sita tu vya wajasiliamali lakini wakati anafanya ziara alikuwa anawahamasisha akinamama, vijana na wazee waunde vikundi na sasa hivi Kata hiyo hadi sasa kuna vikundi 26.

Nassoro alisema kuwa aliwahakikishia wananchi hao waunde vikundi huku gharama zote za usajili atavisimamia yeye Diwani na walifanya hivyo na hadi sasa baadhi ya vikundi zaidi ya 12 tayati vimeshasajiliwa kwa ufadhili wa Diwani huyo.

“Kipindi naanza Udiwani kwenye Kata hii ya Vigaeni kuna maeneo ambayo ilikuwa silali usingizi nilikuwa nawaza ni maeneo ya Kisutu kwani kulikuwa na shida ya maji nikasema nitahakikisha nitapigana na tutahakikisha hili tatizo tutalitatua na kweli tulifukua mifereji  yote Kata mzima na sasa hivi hatimaye kwamba maji yanaelekea sehemu inayohusika matatizo yamepungua sana katika maeneo yale ndani ya miaka miwili sijapata simu sasa hivi nalala usingizi, hii ndio kazi ya ccm ambayo wametuagiza wananchi tuwatekelezee,” alisema Nassoro.

Diwani huyo alisema kuwa pamoja na mambo yote alisema hili kuwainua kinamama na vijana kuna mfuko wa vijana na akinamama wameweza kuusimamia katika Kata ya Vigaeni zaidi ya vikundi saba sasa hivi vimekopa katika halmashauri yao na wamekopa na wengine wameweza kurejesha fedha kwa wakati.

“Niwapongeze sana akinamama kwani baadhi yao wameweza kurejesha fedha kwa wakati na vikundi vinawasaidia tofauti na zamani walivyokuwa wanapata shida wakati ule wa Pride lakini mikopo hii aina masharti magumu wanajianda wenyewe na mambo mengine yanaenda.

Kwa upande wake Ali Chitanda mwanachama wa CCM, aliwataka wananchi mkoani Mtwara, wasidanganyike  na wanasiasa wababaishaji eti wasipigie katiba mpya, naomba pigieni kura katiba mpya kwa nguvu zenu zote ili muweze kuwapigia kura Madiwani, Wabunge na Rais ili CCM iweze kushinda kwa kishindo.
 Mwisho.





TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top