TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Tanzania Bara, John Mnyika, ameitaka Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kupanga
tarehe rasmi katika zoezi la kujiandikisha
katika daftari la kudumu la wapiga kura.
Aliyasena hayo leo kwenye kikao cha Kanda ya Kusini CHADEMA
kikao kilichowajumuisha viongozi mbalimbali
wa chama hicho na baadhi ya wanachama kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara.
Alisema tume kwa sasa ina wajibu wa kutangaza tarehe ambayo itatumika wakati wa zoezi hilo
kwa mikoa yote pamoja na wilaya zake badala ya ilivyo hivi sasa ili wananchi wawe na ukweli kuhusu ratiba
kamili ya uandikishwaji.
Kwa mujibu wa Mnyika
alisema hata hivyo mikoa mingine ratiba haijulikani na nchi mzima ratiba
haijulikani bado wanaitaka Tume ijitokeze itangaze ratiba yenye tarehe Kimikoa
na Kiwilaya Watanzania wajiandae kujiandikisha na wajiandikishe kwa wingi ili
waweze kushiriki kwenye uchaguzi
unaofuata wa Wabunge, Madiwani na Rais.
Aidha Mnyika alitumia Fursa hiyo kutoa pongezi kwa uongozi wa
CHADEMA katika mikoa ya Lindi na Mtwara kwa ushindi walioupata katika uchaguzi
wa serikali za mitaa.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD