TANGAZO
Baadhi ya mashabiki wa Ndanda Fc-Nangwanda |
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
Timu ya Ndanda FC ya mkoani Mtwara,
imeendelea kuwapandisha ugojwa wa moyo wapenzi na mashabiki wa timu hiyo baada
ya kutoka sare ya 0-0 kwenye mchezo wa mashindano ya Vodacom Tanzania Bara,
uliowakutanisha timu hiyo pamoja na timu ya Tanzania Prisons, mchezo uliochezwa
kwenye uwanja wa Nangwanda Sijaona mkoani hapa.
Katika mchezo huo timu ya Ndanda fc
kipindi cha kwanza na cha pili walishambulia sana lango la Tanzania Prisons
lakini hawakubahatika kupata bao licha ya kupata nafasi nyingi za wazi lakini
walishindwa kuzitumia nafasi hizo mpaka mchezo unamalizika timu zote
mbili zilitoka uwanjani bila kutambiana kwa kutoka 0-0.
Katika kipindi cha pili wachezaji
wa Prisons walionekana wakiumia kila baada ya dakika kadhaa kitendo
kilichowakera mashabiki wa timu ya Ndanda na kuanza kuwazomea huku wakiwaambia
wamezidiwa na mchezo huo.
Akizungumza na Blog
ya Mtazamo Mpya, mara baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Rashidi
Mwarabu, mkazi wa India Kotazi, alisema wanaipenda timu yao ndio maana
inapocheza uwanja wa nyumbani wamekuwa wakijitokeza kwa wingi uwanjani kuangalia mchezo lakini imekuwa
ikiwakatisha tamaa kutokana na matokeo inayopata timu hiyo.
“Hii timu yetu inatufanya tuugue
ugonjwa wa moyo inapocheza uwanja wa nyumbani kwa nini hawatupi raha mashabiki
siku zote timu inapocheza nyumbani inatakiwa iwafurahishe mashabiki wake
lakini si kwa Ndanda inatufanya tuugue ugonjwa wa moyo kwa sababu mimi najua
unapokuwa ugenini ukitoa sare ni ushindi kwa timu ngeni sio nyumbani utoke sare
ni aibu.
“Ndanda ikiendelea kufanya hivi
watatufanya mashabiki tusije uwanjani inapocheza katika uwanja wa nyumbani kwa
sababu wanatukatisha tamaa kabisa wakati nyumbani ndiko kwa kufurahia ushindi
kiukweli wanatuumiza kweli mashabiki wao.
Kwa upande wake Abdallah Juma, mkazi wa
Magomeni, alisema kuwa timu hiyo ya
Ndanda inapocheza nyumbani itawafanya mashabiki wasiende uwanjani kuiangalia
kwa sababu tu wamekuwa wakiwakatisha tamaa.
“Watu tulikuwa wengi uwanjani kwa kujua
timu tunayocheza nayo haina uwezo wowote lazima tutashinda ndio maana
tukajitokeza kwa wingi kuja kushuhudia ushindi wa nyumbani lakini imekuwa
tofauti kwa timu yetu…Ndanda kwenye uwanja wa nyumbani kushinda kwao imekuwa
kutoka sare badala ya kushinda hii inatutia uchungu sana na wasipoangalia
wanaweza kushuka daraja.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD