TANGAZO
Katika kufanikisha zoezi la ujenzi wa maabara unakamilika kwa
muda uliopangwa Mbunge wa viti Maalum mkoani Mtwara Anastazia Wambura, ametoa
msaada wa mifuko ya saruji 100 yenye thamani ya shilingi milioni moja na laki
tano kwa ajili ya ujenzi huo katika wilaya ya Mtwara.
Akikabidhi msaada huo mwishoni mwa wiki kwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Fatuma Ally, Wambura
alisema yeye kama mwananchi ameguswa na uchangiaji wa ujenzi wa maabara ambao
kila Mtanzania ana wajibu wa kuchangia
kwa lengo kuhakikisha kunakua na maabara
za kutosha kila shule ya sekondari Nchini.
Alisema ili kupata wataalamu wa masomo ya sayansi watakaokuja kufanya kazi kwenye viwanda vya
gesi na mafuta vinavyojengwa mkoani humo ni vyema kila mwananchi wa mkoa wa
Mtwara bila kujali nafasi aliyonayo lazima achangie ujenzi wa maabara.
Kwa mujibu wa Wambura alisema ujenzi wa maabara unahitaji mchango wa Watanzania wote kwa lengo
la kuhakikisha kunakuwa na maabara za
kutosha na kwamba yeye ni miongoni mwa wakazi wa mkoa huo walioitikia mwito wa
kusaidia ujenzi wa maabara hizo.
“Naomba sana wana Mtwara
pamoja na ujenzi wa maabara tuwasisitize vijana wetu wapende kusoma masomo haya
ya sayansi na hasa kwa kuzingatia mapinduzi ya kiuchumi ambayo yameingia katika
mkoa wetu tumeona viwanda vimeshaanza kujengwa watahitaji waatalamu wa sayansi
ili waweze kuwaajiri”.alisema Wambura.
Kwa upande wake Mkuu wa wilaya ya Mtwara Fatuma Ally, alimshukuru
mbunge huyo kwa kuona umuhimu wa kuchangia ujenzi wa mabaara kwa kutoa mifuko
100 ya saruji ambayo itasaidia sehemu iliyobakia huku akiwataka wadau wengine
kuwa na moyo wa kuchangia ujenzi huo.
Nae Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Selemani Mtalika,
aliwataka wananchi mkoani humo kulipokea kwa nguvu moja suala hilo la ujenzi wa
maabara kwa kuchangia kile walichonacho ili kuendana na kasi ya ujenzi wa viwanda
mkoani Mtwara kulikotakana na ugunduzi wa gesi asilia.
Mwisho.
MBUNGE WA VITI MAALUM KUPITIA CHAMA CHA
MAPINDUZI CCM MKOA WA MTWARA, ANASTANSIA WAMBURA, AKIKABIDHI MIFUKO YA SARUJI 100 KWA MKUU WA
WILAYA YA MTWARA, FATUMA ALLY WA PILI KUTOKA KUSHOTO, WA MWISHO KUTOKA KULIA NI
MEYA WA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI, SELEMANI MTALIKA NA WA MWISHO KUTOKA
KUSHOTO NI ERNEST MWONGI, KAIMU MKURUGENZI WA MANISPAA YA MTWARA MIKINDANI.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD