Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

TANGAZO LA MALIPO YA LESENI KWA WAFANYABIASHARA WA MADUKA YA VILEO MJINI MASASI...

TANGAZO
MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI WA MASASI MKOANI MTWARA ANAWATANGAZIA WAFANYABIASHARA WOTE WA MADUKA YA VILEO (VINYWAJI) KUWA:
LESENI ZA VILEO ZIKO TAYARI NA ZIMEANZWA KUTOLEWA TANGU TAREHE 01/04/2015 NA MWISHO WA KUTOLEWA LESENI HIZO NI TAREHE 24/04/2015 SIKU YA IJUMAA SAA 10:00 JIONI.
BAADA YA KIPINDI HICHO KILICHOWEKWA MSAKO MKALI UTAFANYIKA DUKA KWA DUKA ILI KUBAINI WALE WOTE AMBAO WATAKUWA BADO HAWAJALIPIA LESENI HIZO IKIWA NI PAMOJA NA KULIPA FAINI NA KUFUNGIWA BIASHARA YAKO YA VILEO.
HII NI KWA MUJIBU WA SHERIA YA VILEO YA MWAKA 1968 KIFUNGU NAMBA 28.
AIDHA MGANGA MKUU WA HOSPITALI YA MKOMAINDO MASASI ANAWATANGAZIA WAHUDUMU WOTE WA MADUKA YA VILEO (BAR&GROCERY), NYUMBA ZA KULALA WAGENI PAMOJA NA MAMA LISHE WOTE KUWA WAENDE HOSPITALINI HAPO KUANZIA JUMATATU KWA AJILI YA KUPIMA AFYA ZAO ILI WAWEZE KUPATIWA VYETI VYA KUTOLEA HUDUMA HIZO MUHIMU KWA AFYA ZA BINADAMU.
MKURUGENZI WA MJI WA MASASI PIA ANAWAKUMBUSHA WAFANYABIASHARA AMBAO HAWAJALIPIA LESENI ZAO NA WALE AMBAO HAWANA KABISA LESENI ZA BIASHARA ZAO KUFIKA OFISI YA BIASHARA ZILIZOPO NYUMA YA JENGO LA OFISI YA IDARA YA ELIMU MSINGI KWA AJILI YA KUJA KULIPIA LESSENI AMA KUPEWA LESENI MPYA KWA WALE AMBAO HAWANA KABISA.

TANGAZO HILI LIMETOLEWA NA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MJI MASASI.
             LIPA KODI ZA LESENI KWA MAENDELEO YA MJI WA MASASI.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top