TANGAZO
Na Clarence Chilumba,Newala.
Watanzania wameaswa
kutodharau utamaduni wao na badala yake waache kuiga mambo ya mataifa ya
magharibi kwa kufuata tamaduni za mataifa mengine ili kulinda na kudumisha mila
na desturi za watanzania.
Hayo yalisemwa jana
na kaimu ofisa utamaduni wa Halmashauri ya wilaya ya Newala mkoani Mtwara Sylvester
Chilyenga wakati wa mahojiano maalumu na Blog ya
Mtazamo Mpya ambapo alisema iko tabia iliyoibuka kwa vijana kudai kuwa
kushiriki katika shughuli za ngoma za asili ni kupitwa na wakati.
Alisema tatizo kubwa
lililopo kwa sasa nchini ni kwa baadhi ya watu kuiga mambo mengi kutoka kwenye mitandao ya kijamii
ikiwemo face book,Twitter,instagramu mazingira yanayopelekea baadhi ya ngoma za
makabila ya kusini kuachwa.
“Vijana wengi
wanadharau sana ngoma za asili na kwamba ukiwaambia masuala ya ngoma hawakuelewi
kwani wengi wanaiga mambo ya utandawazi na wale wanaofuata mila na desturi za
kitanzania huwambiwa kuwa wamepitwa na wakati”.alisema.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD