TANGAZO
Na
Clarence Chilumba,Masasi.
Wilaya
ya Masasi mkoani Mtwara imepokea vifaa vya uboreshaji wa daftari la kudumu la
wapiga kura kwa njia ya mfumo wa Kielektroniki (BVR) vyenye lengo la
kuandikisha wapiga kura kwa ajili ya zoezi la uchaguzi wa Rais,wabunge na
madiwani linalotarajia kufanyika Oktoba mwaka huu.
Vifaa
vilivyopokelewa ni pamoja na BVR KIT 84,Stendi za Kamera,Vifaa vya stationary
zikiwemo karatasi,bahasha na fomu mbalimbali,kofia,Tshirt,mabegi ya kubebea
vifaa pamoja na karatasi zitakazotumika kujaza taarifa za mtu atakayekuja
kujiandikisha (ICR FORM).
Wakizungumza
kwa nyakati tofauti kwa niaba ya wakurugenzi wao, Tatu Kazibure ambaye ni Ofisa
Uchaguzi wa Halmashauri ya wilaya ya Masasi na Shaibu Mwakatika ofisa uchaguzi
wa Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara walisema kupokelewa kwa vifaa
hivyo ni ushuhuda kuwa zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
litaanza mapema mwishoni mwa wiki hii.
Kazibure
alisema Halmashauri ya wilaya ya Masasi imepokea jumla ya KIT 56 huku mahitaji
yakiwa ni KIT 80 ambapo alisema wanatarajia kupokea KIT 24 zilizosalia wakati
wowote kutoka sasa ili kuendana na muda uliowekwa wa zoezi la uandikishaji.
Kwa
upande wake Shaibu Mwakatika ambaye ni Ofisa uchaguzi Halmashauri ya mji wa
Masasi alisema wao wamepokea BVR KIT 28 ambapo mahitaji yao ni 32 na kwamba
alikiri kuwa wakati wowote wanaweza kupokea BVR KIT zilizosalia.
Kwa
mujibu wa Mwakatika alisema Halmashauri zote mbili zinategemea kuanza semina
elekezi kwa waandikishaji kesho jumatano April 22 kwa muda wa siku mbili ambapo
zoezi kamili la uandikishaji linatarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii.
Kwa
ujumla wilaya ya Masasi yenye Halmashauri mbili ina jumla ya vituo 112
vitakavyotumika wakati wa uandikishaji ambapo vituo 80 kati ya hivyo ni vile
vya Halmashauri ya wilaya ya Masasi na vituo 32 ni vya Halmashauri ya mji wa Masasi
mkoani Mtwara.
Nao
baadhi ya wananchi wilayani hapa waliohojiwa na Blog ya Mtazamo Mpya walisema
kuwa wamejiandaa kujitokeza kwa wingi kwenye zoezi la uboreshaji wa daftari la
kudumu la wapiga kura ili waweze kushiriki kikamilifu katika zoezi la upigaji kura
kwa katiba inayopendekezwa pamoja na uchaguzi mkuu ujao mwezi oktoba.
Mwisho.
LORI iliyobeba Vifaa Vya Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura Likiwa Nje ya Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi Likishusha vifaa hivyo Tayari kwa zoezi la Uandikishaji linalotarajiwa kuanza mwishoni mwa wiki hii.
MIFUKO iliyohifadhiwa Stendi za Kamera kwa ajili ya Upigaji picha wakati wa Uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura
PICHANI ni BVR KIT zilizopokelewa kutoka tume ya Taifa ya Uchaguzi kwa ajili ya zoezi la uboreshaji wa daftari la kudumu la wapiga kura.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD