Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

DADA ALIYEPIGWA RISASI 3 FEBRUARI 27, 2015 ENEO LA WAPIWAPI MASASI AFARIKI DUNIA HII LEO..

TANGAZO
R.I.P. OUR BELOVED SISTER KABURA.....
#TANZIA: Februari 27 2015 nilitoa taarifa ya Mkazi wa mtaa wa Wapiwapi Halmashauri ya Mji wa Masasi mkoani Mtwara #KABURA #JOSEPH  (35) aliyekuwa  mfanyabiashara  wa vinywaji  katika eneo la Wapiwapi Mjini Masasi ambaye alipigwa risasi tatu  mbili chini ya titi lake la kushoto na nyingine moja mgongoni na watu waliodhaniwa kuwa ni majambazi.
Tukio hilo la #KINYAMA  lilitokea FEBRUARI 26, 2015 majira ya saa 2:30 usiku katika eneo la Wapiwapi karibu na geti la kuingilia nyumbani kwake nyumba  wakati mfanyabiashara huyo alipokuwa akirejea kutoka kwenye biashara zake.
Jeshi la polisi mkoa wa Mtwara lilithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kuwa majambazi hayo yalimvamia mfanyabiashara huyo na kufanikiwa kupora mkoba wake ambao ulikuwa na funguo za dukani pamoja na simu ambazo walifanikiwa kuondoka nazo.
Baada ya Tukio hilo majeruhi huyo alikimbizwa  katika Hospitali ya misheni ya Ndanda Wilayani Masasi na baadaye Hospitali ya Misheni ya Nyangao Mkoani Lindi ambapo kwa mujibunwa taarifa za kipindi hicho zilidai kuwa  madaktari walifanikiwa kutoa risasi zote tatu.

#MSIBA: Kwa Mujibu wa Taarifa rasmi zilizoifikia Blog ya Mtazamo Mpya na kuthibitishwa na mmoja wa ndugu wa karibu wa KABURA JOSEPH zimedai kuwa amefariki dunia hii leo katia hospitali ya Misheni ya Nyangao na kwamba mwili wa marehemu huyo kwa sasa uko katika Hospitali ya Mkoa ya Ligula ukisubiri taratibu zingine za Mazishi. R.I.P.OUR BELOVED SISTER KABURA.......
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top