Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

TAARIFA YA WAZIRI WA KAZI NA AJIRA KWA WAWAKILISHI WA MADEREVA WA MABASI YA ABIRIA..

TANGAZO
TAARIFA YA MKUTANO WA MHE.WAZIRI WA KAZI NA AJIRA NA WAWAKILISHI WA MADEREVA WA MABASI YA ABIRIA, MALORI, TAKSI, PICK UP NA BODABODA.
1. Leo tarehe 9/04/2015,Mhe Waziri wa Kazi na Ajira Bibi Gaudentia Kabaka amekutana kwa muda wa Saa 3 na Wawakilishi na Viongozi wa Madereva wa Mabasi ya Abiria ,Malori ,Taksi, Pick up,na Bodaboda kuhusiana na Tishio la mgomo wa Madereva nchini lililotangazwa na Vyombo vya Habari mwanzoni mwa wiki hii.
2. Kikao hicho kilichofanyika Makao makuu ya Wizara ya Kazi na Ajira kilijadili kwa kina malalamiko mbali mbali yaliyowasilishwa na Wajumbe hao ikiwemo:
• Masuala ya Mikataba ya hali bora kazini kwa Madereva
• Tatizo la ubora wa mikataba ya Ajira kwa Madereva
• Umuhimu wa kuunda chama kimoja cha kusimamia masuala ya Madereva na changamoto zake katika sekta yao ya usafirishaji.
3. Aidha Mhe.Waziri Bibi Gaudencia Kabaka aliahidi kikao kingine na Wawakilishi hao tarehe 18/04/2015 ambapo Mawaziri wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Wizara ya Uchukuzi na Wizara ya Fedha pamoja na Waajiri watashiriki kujadiliana pamoja changamoto mbali mbali zinazohusu Madereva katika sekta hii adhimu ya Usafirishaji
4. Katika kikao hicho cha leo,Mhe.Waziri wa Kazi na Ajira aliwashauri na kuwasihi wajumbe hao kuwaelimisha Wanachama wao kutotumia migomo kama njia ya kuwasilisha matatizo yao kwa kuwa Sheria Na.6 ya Ajira na Mahusiano kazini imebainisha taratibu halali za kufanya mgomo.
5. Waziri Mhe.Gaudentia Kabaka aliahidi kutembelea kituo cha Mabasi ya Mikoani cha Ubungo tarehe 10/04/2015 saa 1 asubuhi kuwataarifu Madereva juu ya kikao cha tarehe 18/04/2015.

Imetolewa
RIDHIWAN WEMA
MSEMAJI
WIZARA YA KAZI NA AJIRA
9/04/2015


TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top