Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

ILI KUMSAIDIA MTOTO HUYU TUMA MCHANGO WAKO KWA NAMBA "0785 101633" ILI AWEZE KWENDA MUHIMBILI HOSP.

TANGAZO
Mtoto SHAILA akiwa na Mama yake
 Na Clarence Antony Chilumba,Masasi.
Mtoto aitwaye SHAILA SHAIBU  mwenye umri wa miezi sita (6) mkazi wa kijiji cha CHIRORO kata ya Namajani Halmashauri ya wilaya ya Masasi Mkoani Mtwara anahitaji msaada wa matibabu katika hospitali ya Rufaa ya Muhimbili kutokana na tatizo  alilonalo la kujaa kwa maji kichwani kulikopelekea kichwa chake kuwa kikubwa.
FEDHA INAYOHITAJIKA KWA AJILI YA UPASUAJI HUO NI SHILINGI MILIONI MOJA NA LAKI MBILI (1,200,000/=) NA WAZAZI HAWANA UWEZO WANAOMBA WACHANGIWE KWENYE NAMBA YA SIMU 0785 101633.
Wazazi wa mtoto huyo wanaitwa SHABANI ABASI MATATA (23) ambaye ni baba na mama ni Penina Maurusi (20) Wote wakiwa ni wakazi wa kijiji cha Chiroro.
Akizungumza na Blog hii Baba mzazi wa mtoto huyo Shabani Abasi alisema mtoto wao alizaliwa akiwa hana tatizo lolote lakini mara baada ya wiki moja kupita tangu kuzaliwa kwake alianza kuona mabadiliko kwenye macho ya mtoto huyo ambayo yalikuwa yanazama kwa ndani.
Alisema walijitahidi kufanya jitihada zote ili kunusuru afya ya mtoto huyo lakini imeshinndikana na hivyo kuamua kufika katika hospitali ya mkuu wa wilaya ya Masasi Bernald Nduta kuomba msaada ili waweze kwenda kutibiwa.
Tatizo hilo hutokana na kuziba kwa mfereji unaopitisha maji ndani ya kichwa na kusambazwa mwilini ambalo kitaalamu hujulikana kama HYDROCEPHALUS na ambalo huwapata watoto kabla na baada ya kuzaliwa kwa watoto walio chini ya umri wa miaka mitano (05).
Akizungumza na Blog ya Mtazamo Mpya Daktari wa hospitali ya Mkomaindo Dr.Kumwembe alisema kuwa tatizo hilo huathiri ukuaji wa mtoto ambaye hushindwa kutembea,kuongea pamoja na kukaa.
Kwa mujibu wa daktari huyo amesema kuwa kwa kuwa hospitali ya mkomaindo Masasi haina vifaa vya upasuaji mtoto huyo amehamishiwa katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili kwa upasuaji utakaogharimu kiasi cha shilingi MILIONI MOJA NA LAKI MBILI (1,200,000/=).
Hivyo kwa yeyote aliyeguswa na tatizo hili anaweza kutuma mchango wake kupitia namba ya simu ya Airtel 0785 101633 ni namba ya Mhasibu wa Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Masasi Mama Anastansia Makunguru.
 Baba Mzazi wa mtoto SHAILA Shabani Abasi Matata akiwa ameshikilia hati ya Rufaa waliyopewa katika hospitali ya Mkomaindo Mjini Masasi inayowataka kwenda katika hospitali ya Muhimbili kwa Matibabu zaidi.
 HATI YA RUFAA KUTOKA HOSPITALI YA MKOMAINDO MASASI.
 Mama Mzazi wa mtoto Shaila  mwenye umri wa miezi sita (6)  Penina Maurusi akiwa amemshikilia mwanae wakiwa katika ofisi za mkuu wa wilaya ya Masasi.
Wazazi wa mtoto Shaila wakiwa kwenye ofisi ya mkuu wa wilaya ya Masasi walipokuja kuomba msaada kutoka kwa wasamaria wema.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top