TANGAZO
Ili kupunguza baadhi ya
changamoto zilizopo katika Hospitali, Zahanati pamoja na vituo vya afya mkoani Mtwara,Serikali
mkoani humo, Imekabidhi vifaa mbalimbali ikiwemo mopu, mashuka, vyandarua
pamoja na mapipa ya taka katika vituo hivyo ili waweze kufanyakazi kwa ufanisi
na kwa uhakika
zaidi.
Akikabidhi vifaa hivyo vilivyotolewa na wadau mbalimbali mkoani
humo wakati wa kilele cha siku ya
wanawake duniani, Mkuu wa mkoa wa Mtwara, Halima Dendego, aliwataka Wakuu wa wilaya mkoani humo, kuhakikisha
wanawashirikiana wadau wote pamoja na
wananchi ili kuweza kusaidia changamoto mbalimbali wanazokumbana nazo katika maeneo yao.
“Naomba nitoe wito hasa kwa Wakuu wa
Wilaya wadau wa maendeleo mnao katika wilaya zenu sisi tumeanza
ebu angalieni fursa hizi mtazitumiaje bajeti yetu ndogo kupitia serikali
haitatusaidia ila tukishirikiana na
wananchi wema katika wilaya na mkoa wetu tunaweza kufanya kitu, kwa hiyo nawaomba wala tusisubiri maadhimisho muda wowote
mna nafasi mna changamoto waiteni washirikisheni watawasaidia katika changamoto
hizo,” alisema Dendego.
Alisema Madaktari wamepewa dhamana ya kule waliko kwenye maeneo yao ya kazi na kwamba
wasiishie tu kuchoma sindano na kutoa dawa kwa wagonjwa bali wakiwa na changamoto watoe taarifa kwa viongozi kwenye
wilaya zao pamoja na wale wa ngazi ya mkoa ili waweze kuyafanyia kazi.
Kwa upande wake Kaimu Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Dkt. Joseph Mwiru, ameshukuru kwa kupata vifaa vya usafi licha ya kukiri kuwa haviwezi kutosheleza kwa matumizi
yote kama hospitali ya Mkoa lakini vitasaidia kupunguza changamoto iliyopo .
“Kiukweli tunashukuru kwa kupata vifaa vya usafi kwa ukweli haviwezi kutosheleza matumizi yote kama hospitali
ya mkoa lakini kwa hiki kidogo
tulichopata hatuna budi kushukuru kwa sababu kidogo ndio mwanzo wa safari.
Hospitali zilizopatiwa msaada huo ni pamoja na Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa Ligula waliopata mashuka 60, vyandarua 88 mapipa ya takataka 20
na tano, Hospitali ya wilaya ya Nanyumbu imepatiwa vyandarua
66 na mapipa ya takataka , Hospitali ya Newala wamepata mashuka 30, vyandarua
80 na mapipa ya taka manane.
Maeneo mengine yaliyopatiwa msaada huo wa vifaa ni pamoja na Kituo cha Afya Likombe kilichopatiwa vyandarua 40 na mapipa ya taka matano ,
Hospitali ya Tandahimba wamepata vyandarua 80 na mapipa ya taka manane, Kituo
cha Afya Nanguruwe wamepata mashuka 21, vyandarua 50 na mapipa ya taka matano, Hospitali ya mji wa Masasi imepata vyandarua 80,mashuka 55 na mapipa ya taka
matano na Hospitali ya Ndanda imepatiwa vyandarua
80 na mapipa ya taka manane.
Mwisho.
Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Halima Dendego (Kushoto) akipeana mkono na Bi. Veronika Kamwenda Afisa Muuguzi Msaidizi wa Hospitali ya Likonde mkoani Mtwara mara baada ya kumkabidhi msaada wa vifaa hivyo.
Halima Dendego mkuu wa mkoa wa Mtwara akimpa mkono Mkuu wa wilaya ya Nanyumbu .
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD