TANGAZO
Na Katuma Masamba.
SERIKALI
imesema ajira za walimu wapya zitaanza rasmi Mei Mosi, mwaka huu huku ikiweka
wazi kuwa walimu hao wasitegemee kupangiwa katika maeneo ya majiji, manispaa na
miji.
Walimu
hao wametakiwa kutotegemea kupangiwa katika maeneo hayo kutokana na idadi ya
walimu waliopo ni kubwa na inakidhi mahitaji, huku maeneo yaliyopewa kipaumbele
ni vijijini na halmashauri ambazo zina mahitaji na upungufu mkubwa wa walimu.
Idadi ya
walimu wapya watakaoanza ajira zao mwezi ujao Ni 31,056 ambapo
Kwa walimu WA ngazi ya Cheti Ni 11,795, Stashahada (Diploma) 6,596 na
wenye Shahada (Degree) 12,665.
Hayo
yameelezwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za
Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini wakati akizungumza na waandishi wa
habari kuhusu ajira mpya za walimu kwa mwaka 2014/2015.
Alisema
kwa mwaka huu ajira hizo zimechelewa kutokana na TAMISEMI pamoja
na Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kufanya ufuatiliaji wa kina hadi katika
ngazi ya shule ili kubaini kwa uhakika mahitaji halisi ya walimu kwa kila
halmahauri na shule.
“Ufuatiliaji
huo umebaini kuwepo kwa halmashauri na shule hasa za mjini zenye walimu wa
ziada na zingine hasa za vijijini zina upungufu mkubwa wa walimu,” alisema
Sagini.
Alisema
taarifa hizo zimesaidia kuwapanga walimu wapya kwa usawa ili kuondoa uwiano
usioridhisha kwenye maeneo mengi ya vijijini. Alisema kwa sasa wanakamilisha
taratibu za kupata kibali kwa ajili ya ajira za walimu na fedha za kuwalipa stahili
zao ili waanze ajira zao rasmi mwezi ujao.
Aidha,
alisema orodha ya walimu na vituo watakavyopangiwa vitawekwa katika tovuti ya
Ofisi ya Waziri Mkuu, TAMISEMI ambayo ni www.pmoralg.com na ya Wizara ya Elimu
www.moe. Go.tz ifikapo Aprili 24, mwaka huu.
Kwa
upande wake Naibu Katibu Mkuu wa TAMISEMI, Zuberi Samataba
alisema, pia ufuatiliaji huo ulikuwa ni kuhakikisha wanakuwa na taarifa sahihi
za walimu wanaoajiri wote ni wapya ambao hawajawahi kuajiriwa ili kuepuka
usumbufu kwa walimu ambao hawatoi taarifa.
Alisema
baadhi ya walimu ambao wameshaajiriwa wanapoenda kusoma, hupangiwa upya vituo
na hawatoi taarifa hivyo kuleta usumbufu wa kuchelewa kutopata mishahara yao.
“Kuna baadhi
ya walimu wameshaajiriwa kwa hiyo jina linapoingizwa katika taratibu za malipo,
linagoma kuingia ndipo ukifuatilia unajua alikuwa ameajiriwa, inabidi umwambie
arudi kwa mwajiri wake.
Kwa hiyo
kwa hawa walimu wapya nawashauri waende kuripoti katika vituo walivyopangiwa na
wakubali kufanya kazi katika maeneo hayo, sio waripoti halafu waondoke,”
alisema.
Wakati
huohuo, Serikali imewataka Makatibu Tawala wa Mikoa ambayo shule zake
zimefungwa kwa madai ya ukosefu wa chakula, kuwachukulia hatua wakuu wa shule
hizo, kwa kile kilichoelezwa kuwa wamekiuka utaratibu kutangaza hivyo ilhali
serikali ilishatuma fedha kwa ajili ya chakula cha wanafunzi katika shule
mbalimbali nchini.
Shule
zilizofungwa kwa tatizo hilo na mikoa yake kwenye mabano ni Rugambwa, Kahororo,
Nyakato na Ihungo (Kagera), Lyamungo (Kilimanjaro), Mpwapwa na Abeid Karume (Dodoma),
Kazima, Milambo, Wavulana Tabora na Wasichana Tabora (Tabora).
Uamuzi
huo umetangazwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na
Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Jumanne Sagini aliyesema serikali imeshatoa asilimia 66.7 ambazo
ni Sh bilioni 28.1 zilizotengwa kwa mwaka 2014/2015.
Alisema
serikali imetoa fedha hizo katika kipindi cha mwezi Julai mwaka jana hadi Machi
mwaka huu kwa ajili ya chakula cha wanafunzi wa shule za sekondari,
zinazomilikiwa na serikali. Sagini alisema serikali ilitenga Sh bilioni
42.1 Kwa mwaka 2014/2015, ambapo kati ya fedha hizo kiasi kilichobaki Ni Sh bilioni
13.9, sawa na asilimia 33.23 ya fedha zilizotengwa.
“Kwa
ufupi, serikali haijafunga shule na wakuu wa shule waliotangaza kufunga shule
hizo chache wamefanya makosa kwa kuwa hawakuwasiliana na mamlaka husika ili
kupata kibali kama kungekuwa na sababu ya kufanya hivyo, naamini mamlaka husika
zitawachukulia hatua,” alisema Sagini.
Alisema
wamiliki wa shule ni Mamlaka za Serikali za Mitaa, ambazo watendaji wake ni
wakurugenzi na wakuu wa shule ni viongozi wasimamizi wa shule hizo, hivyo
hawana mamlaka ya kutangaza kufunga shule kwa sababu yoyote bila kibali cha
mwenye shule.
Kwa
mujibu wa Sagini, kuna utaratibu wa kufunga shule ambapo katika kipindi hiki,
shule nyingi zilikuwa zimefungwa kwa mapumziko mafupi kati ya Machi 28
hadi Aprili 12, ambapo katika shule hizo zilizofungwa wanafunzi
walilazimika kurudi makwao kutokana na kutangaziwa na wakuu wao wa shule.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD