TANGAZO
Na Christopher Lilai,Liwale.
Watu wenye walemavu wa Wilaya ya Liwale Mkoani
Lindi wameiomba Serikali kuwatambua kwa kutenga bajeti kwa
ajili yao kama wanavyofanya kwa vijana na wanawake ili iwasadie katika
kuanzisha miradi midogodogo na kuwafanya waweze kujitegemea na kuachana
na tabia ya kuombaomba mitaani.
Ombi hilo
limetolewa mwishoni mwa wiki na mwenyekiti wa shirikisho la watu wenye ulemavu
wilayani humo Bakari Ngwawile wakati anazungumza kwa niaba ya watu wenye Ulemavu
kwenye tafrija kwa walemavu hao iliyoandaliwa na uongozi wa wilaya
hiyo.
Ngwawile
alisema tabia ya kuombaomba inayofanywa na kundi la watu wenye ulemavu inatokana na
serikali kuliweka pembeni kwa kutokuwezeshwa kiuchumi na kuwa iwapo
kundi hili likiwezeshwa lina uwezo wa kubadilika na kujitegemea hali itakayofanya
kutokuwa na wanaombaomba mitaani.
“Jamii
imekuwa na tabia ya kuwapa vijisenti walemavu wanaoomba mitaani badala ya
kuwawezesha kwa kuwapa mikopo ili waaanzishe biashara ndogondogo”.alisema
Ngwawile.
Alisema kundi hilo limetengwa kwa muda mrefu na
kwamba sasa ipo haja ya serikali kutupia
macho kwenye kundi hilo kama inavyofanya kwenye makundi mengine ya
wazee,vijana,na wanawake.
Alisema
walemavu wilayani liwale wapo zaidi ya 560 lakini takwimu hiyo sio halisi
kutokana na kutofanyiwa sensa ya mara kwa mara pamoja na kutowashirikisha
walemavu kwenye zoezi la utambuzi wa kaya zenye walemavu.
Mwenyekiti
huyo alisema ipo dhana iliyojengeka katika jamii ya kudai kuwa kundi hili
halina uwezo wa kufanya jambo lolote la maana la kuleta tija kwa taifa jambo ambalo
si sahihi na kuitaka jamii kuwaona walemavu sawa na watu wengine kwani wana uwezo
wa kufanya jambo lolote lile kwa ufanisi kuliko hata mtu asiye na ulemavu
kikubwa ni kuwajengea uwezo.
Kwenye
risala yao iliyosomwa wakati wa tafrija hiyo na katibu wa shirikisho la watu
wenye ulemavu, shaibu Jika walemavu hao waliupongeza uongozi wa wilaya
hiyo kwa kuandaa tafrija hiyo ambayo iliwawezesha kuwakutanisha na kushiriki
katika chakula cha pamoja ambapo pia wameweza kufahamiana,kueleza mafanikio na
changamoto zinazowakabili.
Jika
alisema kuwa tafrija hiyo ambayo imekuwakutanisha watu wenye ulemavu
ianzishe sura mpya kwa halmashauri za wilaya kutambua umuhimu wa
kundi hili lilosahaulika katika jamiii.
Walemavu
hao walisema pamoja na kuwepo kwa sera yao ambayo imesainiwa kwa mkataba wa
kimataifa bado kundi hilo linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo uelewa mdogo
wa baadhi ya wazazi juu ya haki za walemavu,ukosefu wa shule rafiki kwa ajili
yao na ukosefu wa mitaji kwa ajili kuendeleza biashara zao.
Changamoto nyingine ni kwa watu wenye ulemavu wa ngozi ambao
wamekuwa wakiuawa kila kona ya nchi na kila kukicha hivyo kuwafanya kuishi maisha
yenye mashaka na kukosekana kwa wawakilishi katika vyombo vya maamuzi katika
ngazi za serikali za mitaa.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya Liwale Humphrey Mmbaga ambaye kwenye
tafirja hiyo alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Lindi,Mwantumu Mahiza ambaye ndiye
alikuwa ndie mgeni wa heshima alisema kuwa lengo la tafrija hiyo ni kuikumbusha
jamii kuwa na utamaduni wa kuwahudumia na kuwaendeleza watu wenye ulemavu
kuanzia ngazi ya familia.
“Tumeamua
kuanzisha sherehe za kuwakutanisha walemavu hao kutokana na kundi hilo kusahaulika
katika jamii kwenye kushirikishwa mambo mbalimbali ya maendeleo na mijumuiko”.alisema
Mmbaga.
Mmbaga
alisema yapo mambo mengi anayoyajua na kutambua kwa kundi hili lakini hayatumiki kutokana na jamii
kuyatenga makundi haya kwa kutambua kuwa hayana msaada wowote.
Aliitaka
jamii inayoishi na walemavu kuwapeleka watoto wenye ulemavu shuleni kwani
ni muhimu kwa kuwa elimu ni dira ya maisha na kuwa mlemavu si kigezo cha kutopelekwa shuleni.
“Ni
jukumu letu wazazi, walezi na washauri kuhakikisha kuwa watoto wenye ulemavu
wenye umri wa kwenda shule wanaandikishwa na kusoma shule kama ilivyo
kwa watoto wengine.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD