Loading...
ADVERTISE WITH US ON THIS BLOG.CALL +255 714 789 592/ +255 682 997 767/ +255 752 944 022

SOMA HOTUBA YA MWENYEKITI WA CHAMA CHA WAANDISHI WA HABARI MKOA WA LINDI....

TANGAZO
Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi Wa Habari Mkoa wa Lindi Abdulaziz Ahmed ambaye pia ametangaza nia ya kuwania nafasi ya ubunge Jimbo la Lindi Mjini kwa tiketi ya CCM.

























Habari za muda huu wanahabari wenzangu,waratibu,wawezeshaji na ma T.A.
Naitwa Abdulaziz Ahmed,ni mwandishi wa habari wa kituo cha runinga cha cha chanel ten,ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari wa mkoa wa Lindi.Lakini kwa kuongezea tu mimi ni mbunge mtarajiwa wa jimbo la Lindi mjini,bado kidogo nitaitwa mheshimiwa.

Binafsi nisingependa niwe mwezeshaji katika kikao kazi hiki.Kwani kazi hiyo imekwisha kufanywa na wawezeshaji kwa umahiri na kwa ufanisi mkubwa.
Pia washiriki tulipata nafasi ya kuchangia na kabadilishana uzoefu na hatimae tutaondoka na mikakati kamambe ya kuunga mkono serikali katika mpango wake huu wenye nia njema na adhimu kwetu kama taifa.Kama ilivyolezwa hapa kwamba suala la kupambana na umaskini lisihusishwe na itikadi za vyama wala dini na hata kabila wala rangi na jinsi ya mtu.Kwani umaskini upo kwa watu ambao wapo kwenye makundi hayo bila kuchagua.

Hivyo niwajibu wetu kama kuunga mkono juhudi hizi kupitia kalamu zetu.
Niwashukuru kwa sana TASAF na serikali kwa ujumla wake kwa kutambua sisi waandishi wa habari kama ni sehemu ya mafanikio ya mpango kama tutashirikishwa kikamilifu katika mpango huu.Niwahakikishie tu kwamba tutoa ushirikiano uliotukuka na wenye tija kwa jambo hili.
Watu wa mikoa ya kusini ni masikini hivyo wanakila sababu ya kukwamuliwa kutoka katika hali hiyo ili nao waweze kutoa mchango wao katika maendeleo ya kiuchumi kwao wenye na taifa kwa sasa na miaka ijayo kwa faida ya vizazi vijavyo.

Tumejifunza na kufundishwa mengi na wawezesha kama nilivyotangulia kueleza.Nikiri tu kwamba mengi ya yale niliyojifunza nilikuwa siyajui kabla ya kikao kazi hiki.
Nahali ingendelea kuwa hivyo bila shaka ningekuwa ni miongoni mwa watu wangeandika kinyume na hali halisi yaani upotoshaji.Nashukuru nimewezeshwa uelewa mapema kabla ya kuharibu.
Nimejifunza kuwa kumbe ushirikishaji unaofanywa katika kuwapata kuwapa walengwa,yaani kaya maskini unafaida kubwa.Ikiwa kuepuka viongozi kuteua watu,jambo ambalo lingesababisha kuingizwa kaya zisizo na sifa kwa sababu binafsi hasa za kimaslahi.Hali ambayo ingezua malalamiko na migogoro na kusababisha nia ya kuzifikia kaya 1000000 kukwama.Kwani muda mwingi ungetumika katika kutatua migogoro.

Lakini kwa mfumo na muundo uliopo katika kuwatambua walengwa ni mzuri sana hasa unapoanzia katika ngazi za vitongoji.Ambapo mapendekezo hayo yanapelekwa katika serikali za vijiji na hatimae mikutano mikuu ya vijiji.
Kwa haki awali kabla ya kupata mafunzo haya niliamini kuwa huo ni urasimu usio na sababu za msingi.Ndugu zangu,uongo ukirudiwa kila mara unaweza kubalika na kufanywa ukweli ingawa kiuhalisi uongo unabaki kuwa uongo japokuwa utakuwa umeanza au umeaminiwa nakuanza kuitwa ukweli.

Gharama ya kufuta uongo ni kubwa sana,nadhani niwajibu wetu sasa tukaporudi tukasaidie kufuta   uliopata kuzungumzwa,unaozungumzwa na utakao zungumzwa kuhusiana na mpango huu.Kama tulivyosikia kwamba fedha zinazotumika katika kufanikisha mpango huo zinatolewa na shirika la wajenzi huru yaani free mason ambayo inanasibishwa na shetani (Devils or Satanic).

Nilikuwa sijui kuwa miradi hii niyajamii na TASAF niwawezeshaji tu.Kwani wanaoibua hiyo miradi niwanajamii wenyewe kutokana na vipaumbele na changamoto zilizopo kwenye maeneo yao.Naamini simimi tu bali niwengi kama sio wote walikuwa wanaamini kuwa miradi hii ni mali ya TASAF nakwahiyo tukajikuta kuwa niwashiriki namba moja wakuilamu TASAF na baadhi yetu kudiriki kuandika habari potofu ima kwakutoelewa au kwa utashi na sababu binafsi za mwandishi.
Naamini baada ya kupata elimu hii hatutaweza kufanya makosa ya aina hiyo.Na atakaye fanya atakuwa ameshindika kama ambavyo jiwe linavyoshikana kuiva kwakuchemshwa kwenye maji ya moto.Sio wajibu wangu kutoa  ushuhuda wa mafanikio yaliyopatikana katika mpango huu kwa kaya maskini.Lakini japo kwa uchache niweze kutoa mfano.Hivi juzi tu mimi na mwandishi mwenzangu wa kampuni ya Raia mwema,anayeandikia gazeti la RaiaTanzania.
Tulikwenda wilayani Kilwa nakutembelea vijiji nakuzungumza nawalengwa.Hakika mimi namwenzangu hatuweza kabisa kuamini mafanikio ya mpango huu.Watu wengi wametoa ushuhuda usio na chembe ya shaka kwamba mpango huu umewanufaisha sana.Wengi wao wameanzisha miradi,hasa ya ufugaji kuku kupitia fedha za mpango huu.Yupo mtoto anaumri wa miaka 14 yupo darasa la nne hana mama wala baba anaishi na dada yake tu ambaye pia ni mdogo.

Lakini sasa kupitia mpango huu anasoma bila mashaka na anapata milo kwa wakati.Kwanini hatukuamini? Bila kuficha nikwamba mimi na mwenzangu tuliamini tungekuta changamoto nyingi ambazo zingesababisha mpango huu kufail.Nijambo ambalo hata mratibu na T.A wa wilaya ya Kilwa ambao   ambao walikuwa niwenyeji wetu hawakujua.Kubwa zaidi ni hofu ya kuwepo changamoto zinazotokana na mivutano ya kisiasa iliyopo katika wilaya ile.

Hali ambayo ilitufanya tuamini kwamba ushindani wakisiasa umewaingia wanajamii na kuingiza mpango huu katika ushindani huo na kuathiri mpango huu.Lakini hali ni tofauti kabisa,mambo ni shwari.Sielewi wahusika wa mpango huu wametumia njia gani zilizosababisha mafanikio hayo ktk eneo lenye changamoto hiyo.Majibu wanayo wenyewe lakini mimi mwenyewe na kwaniaba ya mwenzangu tunawapongeza sana.

Wakati nakaribia kufika mwisho wa hotuba yangu nisingependa nimalize bila ya kuwakumbusha wanahabari wenzangu kuona haja ya kuyafanyia kazi kwa vitendo haya tuliyojifunza.Mimi siamini kama serikali imeamua kutuwezesha fedha sisi waandishi wa habari nakuwa ni miongoni mwa kaya maskini,la hasha.Bali nikwa lengo na makusudio maalum kama ilivyoelezwa na wawezeshaji hasa mkurugenzi ambao walikuwa niwenyeji wetu hawakujua.

Kubwa zaidi ni hofu ya kuwepo changamoto zinazotokana na mivutano ya kisiasa iliyopo katika wilaya ile.Hali ambayo ilitufanya tuamini kwamba ushindani wakisiasa umewaingia wanajamii na kuingiza mpango huu katika ushindani huo na kuathiri mpango huu.Lakini hali nitofauti kabisa,mambo ni shwari.Sielewi wahusika wa mpango huu wametumia njia gani zilizosababisha mafanikio hayo ktk eneo lenye changamoto hiyo.Majibu wanayo wenyewe lakini mimi mwenyewe na kwaniaba ya mwenzangu tunawapongeza sana.

Wakati nakaribia kufika mwisho wa hotuba yangu nisingependa nimalize bila ya kuwakumbusha wanahabari wenzangu kuona haja ya kuyafanyia kazi kwa vitendo haya tuliyojifunza.Mimi siamini kama serikali imeamua kutuwezesha fedha sisi waandishi wa habari nakuwa ni miongoni mwa kaya maskini,la hasha.
Bali nikwa lengo na makusudio maalum kama ilivyoelezwa na wawezeshaji hasa mkurugenzi ambao walikuwa niwenyeji wetu hawakujua.Kubwa zaidi ni hofu ya kuwepo changamoto zinazotokana na mivutano ya kisiasa iliyopo katika wilaya ile.
Hali ambayo ilitufanya tuamini kwamba ushindani wakisiasa umewaingia wanajamii na kuingiza mpango huu katika ushindani huo na kuathiri mpango huu.Lakini hali nitofauti kabisa,mambo ni shwari.Sielewi wahusika wa mpango huu wametumia njia gani zilizosababisha mafanikio hayo ktk eneo lenye changamoto hiyo.
Majibu wanayo wenyewe lakini mimi mwenyewe na kwaniaba ya mwenzangu tunawapongeza sana.Wakati nakaribia kufika mwisho wa hotuba yangu nisingependa nimalize bila ya kuwakumbusha wanahabari wenzangu kuona haja ya kuyafanyia kazi kwa vitendo haya tuliyojifunza.Mimi siamini kama serikali imeamua kutuwezesha fedha sisi waandishi wa habari nakuwa ni miongoni mwa kaya maskini,la hasha.
Bali nikwa lengo na makusudio maalum kama ilivyoelezwa na wawezeshaji hasa mkurugenzi mtendaji wa TASAF.Nijambo lisilopendeza na lisilofaa na kwa jumla ni aibu kuondoka hapa tukiwa vichwa vitupu na kuacha mafunzo haya katika ukumbi huu.Tumeanza kuona nijinsi gani wengine walivyoshiriki na wengine tulivyohudhuria.
Wapo walioshiriki na tulio hudhuria.Kila mtu atajua mwenyewe kama yupo kundi gani kati ya makundi haya mawili.Tukatoe ushirikiano stahiki katika maeneo yetu kwani mikoa hii nimiongoni mwa mikoa maskini sana na sisi niwengi wetu ni wakazi wa maeneo haya.
Tuwe sehemu ya mapambano haya,tusipotoshe jamii bali tuwe waelimishaji.Tuwe nisehemu ya wasuluhishi pale inapotokea migogoro na changamoto.Mfano mdogo niwahi kushuhudia vurugu ambayo nusura itutie aibu mbele ya wageni ambao ni wafadhili waliokuwamekilisha mashirika mbalimbali ikiwamo WORLD BANK,I.L.O, UNDP na mengine walikuja kushuhudia utekelezaji wa mradi huu.
Ilikuwa pale Kiwalala wakati wakugawa fedha kwa kaya maskini.Nilikuwa na na mwandishi mwenzangu huyu huyu niliyeongozana nae Kilwa hivi juzi.Mbele ya wafadhili na watendaji wa TASAF  makao makuu,baadhi ya wananchi kwa makusudi walianzisha vurugu zisizo na kichwa wala miguu.Sababu kubwa walikuwa wanadai zoezi lilifanyika kwa upendeleo na kwamba fedha zile ni kwa ajili ya wazee wote.
Lakini walipoulizwa hatua zilizotumika kuwatambua walengwa walikiri zilifuatwa zote.Hata hivyo baadhi yao walikuwa hawaelewi kwani walihusisha mpango huo na itikadi za siasa.Ilibidi sisiwaandishi  tufanye kazi ya ziada kuwaelimisha wananchi.
Tukagawana makundi,wale wenye misimamo ya siasa walishugulikiwa na mwandishi mwenzangu Mmow,maana yeye hajambo kwenye siasa kiasi cha kuwa na mraba wake kwenye gazeti analoandikia.Mimi nikashugulika na wale waliokuwa wanafuata mkumbo.Tulifanikiwa kutuliza munkari na mambo yalikwenda sawa.
Ndivyo tunavyotakiwa kuwa.Kama tusingekuwa makini basi zile vurugu ingekuwa ni stori ya kuchomoka nayo.Mwisho kabisa nitumie fursa hii kuwaaga  rasmi kwa nafasi ya uenyekiti.Kwani katika uchaguzi ujao sitogombea.Maana kama nilivyotangulia kueleza kwamba natarajia kuomba ridhaa ya chama cha ili niteuliwe kugombea ubunge wa jimbo la Lindi mjini.
Nitaendelea kushirikiana nanyi kama mwandishi wa habari na kushiriki kikamilifu katika mapambano haya ya kuondoa umaskini miongoni mwa wananchi.

Ahsanteni sana kwa kunisikiliza.



TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD
Newer Posts Older Posts
© Copyright Mtazamo Mpya | Designed By FAHARI YA TANZANIA
Back To Top