TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
WAANDISHI wa habari mkoani Mtwara,
wametakiwa kuzingatia na kufuata maadili ya taaluma zao ili waweze kufanya kazi
zao kiufanisi bila matatizo yeyote.
Hayo yalisemwa mwishoni mwa wiki na
Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Mtwara (MTPC), Hassani
Simba, kwenye majumuisho ya Kikao kazi cha waandishi wa habari kutoka mikoa ya
Lindi na Mtwara na Watendaji wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kilichoandaliwa
na TASAF.
Alisema suala la maadili kwa
ajili ya waandishi wa habari ni jambo la msingi kwa kila mwandishi wa habari
aliyopo kwenye taaluma hiyo na kwamba
anapaswa kuzingatia na kufuata maadili ya taaluma yake.
“Suala la maadili kwa ajili ya
waandishi wa habari ni jambo la msingi sana kila mwandishi wa habari aliyopo
kwenye taaluma hii na anafanya shughuli zake ni lazima azingatie maadili kama
yalivyo, kwa sababu vinginevyo mambo mengi yanaweza kutokea taaluma inaweza kudharaulika
lakini pia umma tutaupotosha,” alisema Simba na kuongeza:
“Kwa sababu kwenye maadili kuna mambo
mengi sana mambo ambayo mwandishi wa habari akiyafanya ambayo ni kinyume, jamii
itawaiga…Kwa sababu ukipita sehemu utakuta kundi kubwa la watu wanabishana
ukiwauliza hizo habari umesikia wapi watakujibu tumesikia kwenye magazeti au
radio na tv, kwaiyo waandishi tuzingatie maadili tusije kuipotosha jamii kwani
inatutegemea sisi tuwape habari nzuri na muonekano wa mavazi yetu.
Kwa upande wake Ahmad Mmow, mwandishi
wa habari wa gazeti la Raia Mwema, alisema kuwa kwa ujumla kwa mwandishi yeyote
anatakiwa kulijua hilo kinachofanyika hapa wanakumbushwa tu na kama kuna watu
wanakiuka maadili wanafanya makusudi tu lakini ni jambo ambalo kwa mwanahabari
makini anatakiwa kujua, kuzingatia maadili miongoni mwake kutopendelea,
kutovutwa na vishawaishi na mwisho wa siku kutenda haki kwa watu wote bila
ubaguzi wowote.
Mkurugenzi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii nchini TASAF Bwana Ladislaus Mwamanga (aliyekaa katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na waandishi wa habari wa mikoa ya Lindi na Mtwara wakati wa kikao kazi cha waandishi hao na maofisa wa TASAF kilichofanyika mkoani Mtwara.
Sospeter Magumba ni mwandishi wa
habari na mtangazaji wa Redio Safari mkoani Mtwara, yeye alisema kuwa kimsingi suala ya maadili ya uandishi wa
habari ni kitu ambacho wanapewa mwanzoni kabisa wakati unapoingia chuo cha
uandishi wa habari.
Alisema eneo la uandishi wa habari na
maadili ni kitu cha msingi zaidi kwa sababu kazi yao ni kazi ambayo inabeba
maslahi ya jamii lakini pia inatengeneza ustawi wa jamii, kwa hiyo kwa kawaida
msingi wa maadili ndio unakuwa msingi zaidi ili mwandishi abaki kuwa salama na
amani yake.
Clarence Chilumba ni Mwandishi wa
habari wa magazeti ya Uhuru na Habari leo wilayani Masasi, mkoani Mtwara,
alisema kuhusu alichoongea Mwenyekiti wa Chama cha waandishi wa habari, mkoani
Mtwara (MTPC), Hassani Simba,kuhusiana na maadili ni kweli kabisa kwani
kumekuwepo na tatizo kwani wapo waandishi wengi wamekuwa wakikiuka
maadili tofauti na taaluma zao.
Chilumba alisema kwa mfano mtu
anavyoenda kufanya mahojiano na viongozi hata wakati wa kawaida pia kwenye
suala la mavazi waandishi wengi wamekuwa wakivaa mavazi yanayoenda kinyume na maadili yao.
Alisema siku zote jamii inawangalia
wao kama ni kioo cha jamii sasa wanavyokiuka maadili yao jamii inaweza ikaiga
kutoka kwao“Waandishi wa habari ni kama kioo cha jamii kama ilivyo taaluma
nyingine kama walimu na watu wengine kwa hiyo mwandishi anapokuwa anafanya
tofauti na matarajio ya wengi hilo ni tatizo.
Hata hivyo Chilumba alisema hata
suala la lugha ni tatizo kwao kwani wanavyoenda kufanya mahojiano na watu
waangalie sana makundi kwa mfano watoto wenye matatizo maalumu, majeruhi pamoja
na watu waliofiwa wanatakiwa watumie
lugha ya busara hili wasiwakwaze wale watu ambao wanaenda kufanya mahojiano
nao.
Bwana LADISLAUS MWAMANGA mkurugenzi wa TASAF akiwa kwenye picha ya pamoja na waratibu wa mpango wa kunusuru kaya maskini kutoka wilaya za mikoa ya Lindi na Mtwara.
Bwana Ladislaus Mwamanga ambaye ni mkurugenzi wa TASAF wakati anafungua kikao kazi cha waandishi wa Habari pamoja na maofisa wa TASAF kilichofanyika mkoani Mtwara Kulia kwake ni Mratibu wa TASAF mkoa wa Mtwara Monika Mahundi
Mariam Maregesi ni mwandishi wa
habari wa gazeti la Nipashe, mkoani Mtwara, yeye alisema kwamba suala la
maadili kwa waandishi wa habari wakati mwingine wanaenda ndivyo sivyo kwa
sababu mwandishi anaenda kumuona mtoa habari lakini anaombwa ampatie
muda ili aweze kuandaa taarifa vizuri yeye anataka hiyo taarifa aipate
wakati huo huo kitendo ambacho
hakiwezekani.
Maregesi alisema wakati mwingine
anakuelekeza vizuri lakini mwandishi kwa kujiona kila kitu ndio wewe wamekuwa
wakiwatishia watoa habari kuwa
wataandika anavyojuwa yeye kiukweli hapo wanakuwa wanaenda kinyume na uandishi
wa habari.
Waandishi wa Habari kutoka mikoa ya Lindi na Mtwara wakifuatilia kwa makini hotuba ya mkurugenzi wa TASAF wakati wa kikao kazi kilichofanyika hivi karibuni mkoani Mtwara.
Maregesi alisema wakati mwingine
anakuelekeza vizuri lakini mwandishi kwa kujiona kila kitu ndio wewe wamekuwa
wakiwatishia watoa habari kuwa
wataandika anavyojuwa yeye kiukweli hapo wanakuwa wanaenda kinyume na uandishi
wa habari.
Aidha Maregesi alikemea tatizo la uvaaji mavazi hasa
kwa waandishi wa
Kike,
“Waandishi wa habari hasa wanawake
wamekuwa wakijidhalilisha kwa vyanzo vyao vya habari mwanamke unaenda umevaa nguo ya ajabu sehemu
zako ambazo ni nyeti wakati mwingine zinaonekana ukifika pale unafukuzwa na
yule mtoa habari inakuwa haitujengi isipokuwa inabomoa maadili ya uandishi wa
habari,”alisema Maregesi na kuongeza:
“Unapokuwa kama mwandishi wa habari
ni chombo ambacho watu wengi wanategemea kwa hiyo jamii inategemea kuiga mema
kutoka kwako lakini sasa unavyoenda kwa
chanzo chako cha habari umevaa vibaya unamjengea nini nia yako, kiukweli
kimsingi waandishi wa habari tunatakiwa sana tuzingatie maadili yetu hili na sisi
tuweze kuheshimika kwa vyanzo vyetu vya habari na jamii kwa ujumla.
Mwisho.
Picha ya pamoja kati ya Mkurugenzi wa TASAF pamoja na Baadhi ya wataalamu Washauri wa TASAF.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD