TANGAZO
Na Fatuma Maumba,Mtwara.
WAANDISHI wa habari kutoka
mikoa ya Lindi na Mtwara, wamewataka Waratibu wa Mfuko wa maendeleo ya
Jamii(TASAF) kuwashirikisha wanahabari pindi wanapoenda vijijini
kutembelea miradi wanayoisimamia katika maeneo husuka.
Hayo yalisemwa jana na Mwandishi wa
habari wa kituo cha televisheni cha Channel Ten, John Kasembe, kwenye kikao
kazi cha waratibu pamoja na waandishi wa habari kuhusu Mpango wa
kunusuru Kaya maskini unaotekelezwa na Tasaf awamu ya tatu.
alisema Waratibu wengi
wanapoenda vijijini kufatilia miradi wanayosimamia wamekuwa wakienda peke
yao bila kuongozana na waandishi wa habari ili waweze kuandika kile
wanachokifanya ili jamii iweze kutambua na kufahamu mpango
unaotekelezwa na mfuko huo.
“TASAF Makao Makuu inabidi
wawasisitize Waratibu jinsi watakavyoweza kushirikiana nao vizuri
waandishi katika wilaya zao ili pale wanapoenda kuomba taarifa au kutaka kujua
kitu fulani basi ionekane wanapata sapoti ya pamoja hii itaonesha kwamba sasa
ukweli na uwazi ulipo, kwa sababu mwandishi wa habari usipomshirikisha yeye ana
nyenzo nyingi za kupata habari”.alisema.
Kwa upande wake mwandishi wa habari
wa gazeti la Mwananchi, Abdallaa Nassoro, alisema wao kama waandishi wa habari
kupata mafunzo hayo ni muhimu sana kwa sababu yatawasaidia kupunguza mianya ya
upatikanaji wa habari na utoaji wa habari sahihi.
“Kumbuka waandishi wa habari hawaoti
mambo lazima wafahamu kwa undani na waandishi wa habari kufahamu utekelezaji wa
miradi ya TASAF kwa undani itasaidia sasa katika upashanaji wa habari sahihi
zinazohusu utekelezaji wa miradi hiyo… Inatuwia vigumu sana waandishi wa habari
kuripoti habari ambazo kwa wakati mwingine hatuzifahamu kwa kina kwa hiyo
kuwepo kwa mafunzo haya kwetu ni faraja na tutafungua ukurasa mpya kwa maana
waandishi wa habari watakuuwa wanafahamu juu ya shughli mbalimbali
zinazotekelezwa na TASAF.
Naye Mtaalamu wa Mawasiliano kutoka
TASAF Makao Makuu, Zuhura Mdungi, alisema lengo kubwa la kikao hicho na
waandishi wa habari ni kujenga mahusiano mazuri katika kazi ili kuweza
kuelimisha jamii juu ya mpango wa kunusuru Kaya maskini na jinsi ambavyo
umeweza kusaidia ile Kaya maskini katika kujitoa kwenye umaskini.
Hata hivyo Mdungi, amewataka Waratibu
hao wa TASAF kuona umuhimu wa kuwahusisha Wakurugenzi wa halmashauri moja kwa
moja ili waweze kufahamu vizuri kuhusiana na utekelezaji wa mpango huu.
Alisema waratibu wa TASAF katika halmashauri wawe na utamaduni wa
kuwashirikisha Wakurugenzi wa halmashauri moja kwa moja ili waweze kufahamu
vizuri kuhusiana na utekelezaji wa mpango huu.
“Tunaelewa Wakurugenzi wana shughuli
nyingi lakini ni muhimu wakashiriki kufika katika eneo husika kushuhudia shughuli
mbalimbali ambazo zinafanyika kwa walengwa”. Alisema Mdungi.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD