TANGAZO
Na Fatuma Maumba, Mtwara.
JUMUIYA ya Vijana wa Chama cha
Wananchi CUF, Mtwara mjini, wameladhimika kupiga kambi kwenye Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa Ligula ili kufanya usafi kwenye eneo la wodi ya wazazi
kutokana na eneo hilo kuzungukwa na nyasi ambapo inaweza kuleta madhara kwa
kuwa madhalia ya mbu na kusababisha ugonjwa wa malaria.
Akizungumza na Blog ya Mtazamo Mpya,mara baada ya
kumalizika kwa usafi, Katibu wa Jumuiya hiyo, Jamali Waziri, alisema wao kama
vijana wamehamasika kwenda kufanya usafi hospitalini hapo baada ya kuona
mazingira yake si mazuri kutokana na kuzidiwa kwa nyasi nyingi hasa kipindi
hiki cha mvua.
“Sisi Kama vijana baada ya
kuzunguka katika maeneo yetu ya Manispaa ya Mtwara-Mikindani tukagundua kuna
maeneo yanahitaji kufanyiwa USAFI hususani maeneo ya Hospitali ya Rufaa ya Mkoa
Ligula kwani tulikuta mazingira ni machafu ambayo yanahitajika kufanyiwa usafi.
Kwa mujibu wa Katibu huyo alisema
uchafu wake ambao walikuta kwenye hospitali hiyo inatokana na uoto wa nyasi na wao kama vijana wakaamua
kufanya usafi ili kuweka mazingira safi na salama, lakini hawataishia hapo tu
kuna maeneo mengi wameyazungukia na yanahitaji kuwekwa sawa.
Alisema mfano kuna maeneo mengine
mengi ni machafu kuna barabara za mitaa hazijafanyiwa kazi wamejipanga
kutembelea kwenda kuweka sawa kwa kufanya usafi kwenye mitaro kadri
watakavyoweza.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mipango
na Uchaguzi (JUVICUF) Mtwara Mjini, Rashidi Athumani, alisema wao kama vijana
walikaa wakaadhimia katika kikao cha kamati tendaji wafanye maadhimio ya
kutembelea katika taasisi za kijamii ili waangalie hali halisi na wao kama
vijana waweze kujitolea nguvu zao pamoja na fedha.
Alisema waliamua kwenda Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa Ligula kwa kuwa mazingira yaliyokuwepo hospitalini hapo si ya
kuridhisha hasa wodi ya akinamama ambao wanaenda kuuguza ndugu zao huku wengi wakilala
nje mazingira ambayo huweza kusababisha kupata maambukizi ya Malaria.
Nae Kaimu Mganga Mfawidhi Hospitali
ya Rufaa ya mkoa Ligula, Dk. Frank Sudai, amewashukuru vijana wa CUF kwa
kujitoa kwenda kufanya usafi kwenye baadhi ya maeneo kwenye hospitali hiyo
kutokana na kuelemewa na nyasi hasa kipindi hiki cha mvua.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD