TANGAZO
Na Clarence
Chilumba,Masasi.
Jeshi la polisi
wilayani Masasi mkoani Mtwara linawashikila watu watatu kwa tuhuma za wizi wa
pikipiki aina ya San Moto mali ya Kampuni ya San Moto wilayani Masasi uliotokea
mwishoni mwa mwezi uliopita.
Tukio hilo lilitokea
mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu katika eneo la Masasi Mbovu ambapo watu
wasiofahamika walivamia duka hilo la kufanikiwa kuiba pikipiki moja aina ya San
moto.
Kaimu mkuu wa jeshi
la polisi wilaya ya Masasi Nathanael Kyando aliwataja wanaoshikiliwa na jeshi
la polisi Masasi kuwa ni pamoja na Abdulaziz Selemani (26) mwalimu wa shule ya
Sekondari wilayani Tandahimba,Ahmad Said (22) mkazi wa Newala pamoja na Sharifu
Bakari ambaye ni mwanafunzi wa sekondari mkazi wa Tandahimba.
Alisema watuhumiwa
hao wanashikiliwa na jeshi la polisi wilaya ya Masasi kwa upelelezi zaidi na
kwamba upelelezi utakapokamilika watafikishwa mahakamani kujibu shitaka linalowakabili.
Ikumbukwe kuwa katika
tukio hilo wananchi wenye hasira walimuua mtu mmoja kwa kupigwa mapanga ambaye
hata hivyo jina lake halikuweza kupatikana kwa madai kuwa yeye ndiye aliyekuwa
amehusika katika tukio hilo la wiz wa pikipiki.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD