TANGAZO
Alhaj Maulana Muhibu Shirazi. |
Na Clarence Chilumba, Masasi.
Alhaj Maulana Muhibu Shirazi (71) wa Jumuiya ya Wiz’yatu LiQadria iliyoko Katika
Kijiji cha Chikundi Halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara anashikiliwa
na jeshi la polisi wilaya ya Masasi kwa tuhuma za kukutwa na watoto wadogo
wapatao 11 kinyume na taratibu na sheria za nchi.
Pia amekutwa na fomu za usajili
zinazoonesha taarifa muhimu za mwanafunzi zikiwemo jina la mtoto, jina la mzazi,
mahali anakotoka kwa maana ya kijiji na kata pamoja na mawasiliano ya mzazi au
mlezi wa mwanafunzi.
Watoto waliokutwa katika kituo hicho (Pichani hapo chini) ambao wanatoka katika maeneo mbalimbali ya mikoa ya Lindi na Mtwara ni pamoja
na SELEMANI JUMA (12) mkazi wa kijiji cha Mandawa wilaya
ya Ruangwa, JAMALI ABASI (12) mkazi wa Mwena Masasi, KARIMU ABBASI (17) mkazi wa wilaya ya
Liwale mkoani Lindi, MARK MUHIDINI (10) mkazi wa kijiji cha Mkululu wilayani
Masasi, NURUDINI AUSI (11) kutoka kijiji cha Mpanyani Masasi
pamoja na ALLY BAKARI (12) mkazi wa kijiji cha Milola mkoani
Lindi.
Wengine waliokutwa nyumbani kwa Alhaj
Huyo ni GANAFI HAMISI (13) kutoka katika kijiji cha Mkululu
Masasi, BAKARI NANG’ANI (12) mkazi wa wilaya ya Ruangwa mkoani
Lindi, HAJI JUMA (18) wa kijiji cha Mkululu wilayani Masasi, MWAJUMA SELEMANI (10) wa kijiji cha
Mwena, MURJI MUHIDINI (12) mkazi wa Mkululu wilaya ya Masasi
pamoja na HAMIS SEIF (05) mkazi wa kijiji cha Kanyimbi
wilayani Masasi katika mkoa wa Mtwara.
Watoto walikoutwa nyumbani kwa Alhaj Maulana Huko katika kijiji cha Chikundi wilayani Masasi mkoani Mtwara wakiwa wamewekwa chini ya ulinzi katika kituo cha polisi wilaya ya Masasi kwa mahojiano zaidi.
Watoto hao wakiwa kituo cha Polisi Masasi baada ya kukutwa kwenye nyumba ya mzee huyo huko Chikundi Masasi.
Jeshi la polisi wilayani Masasi
limethibitisha kutokea kwa tukio kupitia kwa Kaimu mkuu wa jeshi hilo wilaya ya
Masasi NATHANAEL KYANDO na kusema kuwa linamshikilia
mtuhumiwa huyo kwa mahojiano zaidi
Mkuu wa Wilaya ya Masasi BERNALD NDUTA ambaye ni Mwenyekiti wa Kamati Ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya (Mwenye shati la Draft pichani) akiwasili kwenye eneo la tukio kushuhudia namna watoto hao walivyopatikana.
Akiongea na Blog ya Mtazamo Mpya mzee Maulana (Pichani hapo chini) alikiri
kukaa na watoto hao walioletwa na wazazi pamoja na walezi wao kwa zaidi ya
miezi miwili nyumbani hapo kwa madai ya kuwapa elimu ya dini ya Kiislamu kwa
muda wa miaka mitatu ili aweze kupata THAWABU kutoka kwa Mungu kwa kuwa yeye ni
Alhaj.
Alisema hakuwa na
nia mbaya ya kukaa na watoto hao ingawa amekiri kufanya makosa ya kukaa na
watoto ambao walistahili kuwepo shuleni kupata elimu dunia na kuliomba jeshi la
polisi limwachie huru kwa kuwa alichokitenda ni moja ya ahadi ambayo aliihaidi
kuwa ataitimiza mara tu baada ya kurejea kutoka kwenye “IBADA YA HIJJA” aliyoenda mwaka 2013.
Kwa mujibu wa Alhaj
Maulana alisema alianza kukaa na watoto hao Desemba mwaka jana kwa makubaliano na
wazazi wao kuwa masomo chuoni hapo yataanza rasmi Januari 30, 2015 huku moja ya
sharti la chuo likiwa ni mzazi kugharamia matibabu ya mtoto wake pindi
atakapolazwa.
ALHAJ Maulana Muhibu Shiraz (71) wakati anatoa maelezo kwa mkuu wa wilaya ya Masasi (Hayuko pichani) katika kituo cha polisi wilaya ya Masasi kuhusu watoto hao kumi na moja waliokutwa nyumbani kwake huko katika kijiji cha Chikundi.
Hata hivyo katika
hali ya kushangaza ni pale Katibu Tawala wa Wilaya ya Masasi Danford Peter
alipoamua kupiga moja ya namba ya simu ya Mzazi wa mtoto ALLY BAKARI (0783-812523) anayetoka kijiji
cha Milola Lindi aliyefahamika kwa jina la BAKARI MTAPILA ambapo mtu huyo alipokea simu na alikana kuwa jina hilo si lake
na hana mtoto mwenye jina hilo licha ya kukiri kuwa ni mkazi wa Milola.
Fomu ya Kujiunga na Chuo hiko ambayo alikutwa nayo mzee Maulana na ambayo namba iliyopo kwenye fomu hiyo ilikataliwa kuwa si ya muhusika wa namba hiyo.
Kwa upande wake
mkuu wa wilaya ya Masasi ambaye alikuwepo kwenye eneo la tukio BERNALD NDUTA alisema wao kama serikali
wameviagiza vyombo vya dola kufanya utafiti wa kina kuhusu tuhuma hizo na
hatimaye watatoa taarifa rasmi kwa vyombo vya habari.
Naye Ofisa Ustawi
wa Jamii halmashauri ya wilaya ya Masasi mkoani Mtwara THABITI .A. THABITI alisema mzee huyo ametenda kosa la
kukaa na watoto hao ambao amewakosesha haki zao za msingi ikiwemo elimu huku
akikiri kuwa hata mazingira ambayo wanaishi watoto hao si mazuri kwani walikuta
watoto hao wakilala chumba kimoja zaidi ya watoto wanne na mbaya zaidi walikuwa
wanalala chini ya sakafu iliyotandikwa vipande vidogo vya godoro.
Mke wa Alhaj Maulana aitwaye MWANAHAWA HASHIMU (43) (aliyevaa Hijab) akiwa katika kituo cha polisi wilaya ya Masasi.
Hadi Blog ya Mtazamo Mpya inaondoka kwenye kituo cha polisi
wilaya ya Masasi iliacha bado mtuhumiwa huyo aliyeambatana pamoja na mke wake
aliyefahamika kwa jina la MWANAHAWA HASHIMU (43) alikuwa anashikiliwa na jeshi hilo pamoja na watoto hao kwa
mahojiano zaidi.
Tutaendelea kuwajuza
kitakachoendelea………………..
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD