TANGAZO
Na John Kasembe,Tandahimba.
Chama kikuu cha
ushirika wa mazao cha wakulima wa zao la korosho wilaya za Tandahimba na Newala mkoani Mtwara kimepitisha malengo yake ya ukusanyaji
wa zao la korosho katika msimu wa mwaka
2014/15 hali iliyopelekea vyama
hivyo kupata jumla ya shilingi zaidi ya Billioni 127 kwa msimu huu.
Akizungumza na waandishi wa habari mwenyekiti wa Chama
kikuu cha ushirika cha wakulima wa korosho wilaya ya Tandahimba na Newala YUSUF
NANNILA alisema katika msimu huu chama chake kimeweza kukusanya tani 78,000 na
kilogramu 400 zilizosababisha vyama vyake
vya msingi kujipatia jumla ya shilingi Billioni 127 na kugawanywa katika vyama
vyake.
Aidha mwenyekiti huyo
ameeleza kuwa katika makusanyo hayo jumla ya tani 2000 za korosho zimekwama kuingia sokoni
kutokana na korosho hizo kutokuwa na ubora unaostahili kuingia kwenye soko.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD