TANGAZO
Na John
Kasembe,Mtwara.
Makampuniya
uwekezaji yaliyoonesha nia ya kuwekeza katika uvunaji wa rasilimali
zinazopatikana katika mikoa ya kusini ya Lindi, Mtwara pamoja na Ruvuma yametakiwa kuhakikisha yanazingatia
uhifadhi wa mazingira ili kuepusha neema ya uwekezaji huo kugeuka balaa kwa
ustawi wa mazingira.
Mkuu wa Mkoa wa
Ruvuma, Saidi Mwambungu ametoa wito huo jana wakati wa ufunguzi wa jukwaa la maendeleo
endelevu kwa mikoa ya kusini yaliyoandaliwa na shirika la kimataifa la uhifadhi
wa misitu (WWF) yaliyofanyika kwenyeukumbi wa NAF Beach mjini Mtwara.
Alisema makampuni
mengi yameonesha nia ya kuwekeza katika mikoa ya kusini katika uvunaji wa
rasilimali ya gesi, mafuta, madini, uranium na makaa ya mawe na kwamba
uwekezaji huo ni lazima uzingatie uhifadhi wa mazingira.
Kwa upande wake
mratibu wa uhifadhi wa ardhi wa WWF Profesa Husein Sosovele
alibainisha kuwa hakuna maendeleo endelevu yanayopatikana bila ya kuhifadhi
mazingira ya maeneo husika,ambapo ameeleza kuwa bado mazingira ya mikoa ya
kusini hayajaharibiwa kutokana na uwekezaji uliopo.
Mwisho.
TANGAZO
Facebook Blogger Plugin by WAYEGE CO.LTD